Posts

Showing posts from July, 2023

Msimamo wa Nchi ni kulinda Uhuru wa Vyombo vya Habari

Image
 Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhe.Nape Nnauye amesema msimamo wa thabiti wa Nchi ya Tanzania ni kulinda Uhuru wa Vyombo vya Habari,na ndio mana Serikali iliamua kufanya marekebisho ya Sheria ya huduma ya Habari Sura ya 229,ili ikidhi Uhuru wa vyombo vya Habari. Mhe .Nape amesema hayo Leo Julai 31,2023 jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua kozi fupi ya 15 ya Wahariri wa vyombo vya Habari inayotolewa na chuo Cha Taifa Cha Ulinzi. "Wanahabari niwahakikishieni msimamo thabiti wa Nchi yetu ni kulinda Uhuru wa vyombo vya Habari.Mh.Rais mara nyingi amekuwa akiagiza kufanya kazi bila kuingilia Uhuru wa vyombo vya Habari",amesema Mh.Nape. Aidha amewataka Wahariri hao mara watakapomaliza  kozi hiyo na kurudi katika vituo vyao vya  kazi,wafanye kazi kwa kuangalia maslahi ya nchi,vilevile amewataka kuendelea kulifanya Taifa kuwa kitu kimoja na Kukuza Umoja wa Taifa. Kwa upande wake kansela wa chuo Cha Taifa Cha Ulinzi,Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee amesema kuwa mafu

Watumishi Wa Umma Wilayani Kalambo Waungana Kuadhimisha Kumbukizi Ya Mashujaa Kwa Kufanya Usafi.

Image
  Watumishi wa Umma wilayani Kalambo mkoani Rukwa wameungana na watu wengine katika kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya mashujaa kwa kufanya usafi kwenye majengo ya hospitali ya wilaya  hiyo ili kuendeleza kampeni ya usafi wilayani humo. Zoezi hilo liliongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo Lazaro Komba alisisitiza kuwa zoezi hilo ni endelevu kwa kila siku ya mwisho wa mwezi ili kukabiliana na magonjwa ya milipuko ikiwemo kipindupindu na magonjwa ya kuhara. Komba alisisitiza wananchi kujenga mazoea kufanya usafi wa mazingira kuzunguma maeneo yao husika kwa lengo la kuifanya wilaya kuwa safi muda na wakati wote. ‘’Kimsingi leo tumekutana kufanya usafi hapa kwenye majengo ya Hospitali ya wilaya Kalambo kama  sehemu ya kuadhimisha kumbukizi ya siku ya mashujaa na maadhimisho haya kwa ngazi ya kitaifa yanafainyika mkoani Dodoma’’ alisema komba. Mapema akiongea na Watumishi wa umma wakati wa shughuli za usafi kwenye maeneo hayo ,Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Shafi Mpenda alisema

WATOTO WATATU FAMILIA MOJA WAFA MAJI WAKIVUA SAMAKI KATAVI

Image
  Na.Mary Clemence,Katavi Watoto watatu wa familia Lucia Kazima(10),Kabisi Lazima(8),na Makala Lazima(6) wakati wa kitongoji Cha Kayenze B Wilayani Mpanda wamekufa Maji wakati wakivua samaki katika mto Kamilala. Watoto hao walikuwa wanafunzi wa shule ya msingi Kamilala ambapo Lucia alikuwa akisoma darasa la 5,Kabisi darasa la nne na Makala darasa la kwanza. Kamanda wa polisi Mkoa wa Katavi,Kaster Ngonyani akizungumza na Waandishi wa Habari Leo jumatano Julai 19,2023 amesema tukio Hilo limetokea Julai 13,2023 saa 7:45 mchana. "Eneo la mto huo linatumika pia kwa shughuli za uvuvi samaki,watoto hao walikwenda kuvua samaki,haikufahamika kama walikuwa wanaogelea au ilikuwaje,"amesema. "Kwa sababu hii miili Yao ilikutwa ikielea na wasamalia wema walitoa taarifa polisi Kisha iliopolewa na kufanyiwa Uchunguzi Kisha ndugu wakakabidhiwa kwa ajili ya taratibu za maziko,"amesema Kaster. Kamanda Ngonyani ametoa Rai kwa wazazi na walezi kuwa na uangalizi wa karibu pindi watoto wa

HUDUMA YA KITI MWENDO YAANZISHWA KITUO CHA DALADALA MUHIMBILI.

Image
 Hospital ya Muhimbili imeanzisha huduma ya kubeba wagonjwa wasioweza kutembea kutoka kwenye kituo Cha daladala kilichopo nje ya geti la kuingilia hadi katika maeneo ya kutolea huduma kwa kutumia Viti mwendo(wheel chairs). Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za uuguzi na ukunga wa MNH,Bi.Redempta  Matindi amesema kuwa huduma hiyo ni muhimu kwa kuwa wapo wagonjwa wasiojiweza kabisa kutembea wenyewe. "Sisi kama watoa huduma tumeona ni vema kuanzisha huduma hii kuwasaidia mwendo wagonjwa ili wafike kwenye maeneo ya kutolea huduma wakishafika huko wanakutana na watoa huduma wa maeneo husika"amesema Bi Redempta. Amesema huduma hizo zinatolewa na waliokuwa waraibu wa dawa za kulevya ambao wanaendelea na tiba ya Methadone ili kuwasaidia kurejea katika maisha ya kawaida.

KASULU DC YAENDELEZA UUNDAJI WA KLABU ZA LISHE

Image
 Na Mwandishi wetu. Katika kuendelea kuboresha Afya ya Jamii Halmashauri ya Wilaya Kasulu kupitia kwa wataalamu wa lishe inaendelea kuunda Klabu za lishe mashuleni ambazo zitasaidia kutoa Elimu ya masuala ya lishe,kwa kuanzisha bustani za mbogamboga na matunda. Akitoa ripoti hiyo Leo katika kikao Cha lishe kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo Afisa Lishe Kingolo Sayi amesema Hali ya uwepo wa Klabu za lishe ni asilimia 43 kwa shule za msingi na asilimia 75 kwa shule za sekondari. Sayi ameongeza kuwa katika kuimarisha uungwaji wa Klabu hizo mashuleni,vijiji 24 katika kata 15 vimehamasishwa juu ya umuhimu wa Klabu shuleni. Itakumbukwa kuwa uwepo wa Klabu za lishe shuleni zinasaidia kutoa Elimu kwa wanafunzi a jamii juu ya umuhimu wa lishe Bora na ushiriki wake.

HALMASHAURI ZAAGIZWA KUSIMAMIA KUSIMAMIA MIRADI YA BOOST.

Image
 Mkurugenzi TAMISEMI anayeshughulikia masuala ya Elimu Vicent Kayombo amemtaka Maafisa Elimu kwenye Halmashauri zote mkoani Rukwa kusimamia kwa ukaribu ujenzi wa miradi ya madarasa yanayojengwa maarufu kama miradi ya BOOST. Akizungumza na Maafisa Elimu wa ngazi zote mkoani Rukwa Mkurugenzi huyo wa TAMISEMI alisema hajaridhishwa  na kasi ya ujenzi wa miradi hiyo ambayo imekuwa ikitekelezwa pasipo kwenda na wakati. Kayombo ametoa agizo Hilo baada ya kufanya ukaguzi wa baadhi ya majengo na kutoridhishwa na kasi yake ya ujenzi wake.   Hata hivyo licha ya kusisitiza Maafisa Elimu kusimamia majengo hayo ya Boost aliwataka kusimamia huduma Bora kwa walimu kwenye maeneo Yao ya kazi sanjari na kuwasikiliza hoja zao na kuzitafutia ufumbuzi yakiwapo madai Yao na upandaji wa madaraja. Aidha aliwapongeza watendaji wa idara ya Elimu kwa kufanikisha ufaulu mzuri wa wanafunzi katika matokeo ya kidato Cha sita kwa asilimia 99 na kufuta Zero katika mwaka 2023.

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA SUMBAWANGA AFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI YA AFYA NA ELIMU.

Image
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Sumbawanga Bi.Lightness Msemo akiambatana na wataalamu toka ofisini kwake wamefanya ziara ya kukagua miradi ya Elimu na Afya pamoja na kufanya vikao na watumishi wa kata sita  mfinga,Mwadui,Kikwale,Kalumbaleza,Muze,Mtowisa,Zimba na Milepa. Katika ziara hiyo alitembelea shule ya msingi kizumbi iliyopo katika kata ya Muze na kukagua ujenzi wa miundombinu ya vyoo inayoendelea katika shule hiyo.Katika kikao kazi Cha walimu na viongozi wa Kijiji akiwepo Mtendaji na mwenyekiti alisisitiza suala la kuwahi kazini kwa watumishi na kusimamia miradi inayoendelea kujengwa kwa ufanisi ili kuwa na Tija kwa jamii. Pia alifanya ukaguzi katika Kijiji Cha Kasekela kata ya Mfinga baada ya ukaguzi wa mradi Mganga Mkuu wa wilaya Dr.Msuya akitoa Elimu kwa wazazi juu ya lishe Bora na kuwasihi wazazi kuzingatia lishe borakwa watoto ili kupunguza suala la udumavu kwa watoto.Mganga Mkuu aliwasihi wauguzi kuendelea kufanya kazi kwa kujituma ili kuendelea kuokoa maish

MBUNGE WA JIMBO LA KWELA NA MKURUGENZI MANISPAA YA SUMBAWANGA WAONGOZA HARAMBEE UJENZI WA KANISA KATILIKI.

Image
 Mbunge wa Jimbo la Kwela Mheshimiwa Deus Clement Sangu na Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Bi.Catherine Mashallah wameongoza harambee ya ujenzi wa kanisa la parokia ya Mt.Fransisco wa Asiz Jimbo la Sumbawanga. Mbunge wa Jimbo la Kwela Mh.Sangu ametoa kiasi Cha shilingi Milioni tatu  ajili ya ujenzi wa kanisa la parokia hiyo. Mh.Sangu amesema,"Kwa namna nilivyoona parokia hii mnavyojitoa nimefarijika sana mimi kama Mwanaparokia nimewiwa sana naamini MwenyeziMungu ataniwezesha Kila wakati  kuweza kupata nguvu yakuja  kujenga kanisa hili kwa pamoja" Nae Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Bi.Catherine Mashalla amechangia mifuko mia Moja (100) ya saruji katika ujenzi wa kanisa Hilo wakati wa uendeshaji wa harambee ya ujenzi huo,nakuwaambia waumini wa parokia hiyo kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan inafanya Kazi kubwa hivyo ni jukumu letu kuunga mkono mambo yote anayoleta Rais wetu kwa kuyasimamia,kuyatunza na kuyalinda.  Aidha,akitoa

SERIKALI,VIONGOZI WA DINI WATETA LUGHA MALEZI YA WATOTO

Image
 Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, wanawake na Makundi maalumu,John Jingu amesema kuwa migogoro ya kifamilia inachangia watoto kuwa katika Hali mbaya ya MALEZI na kuongeza vitendo vya ukatili kwa watoto. Dkt.Jingu amesema,Takwimu za jeshi la polisi Tanzania kuanzia Januari mpaka disemba 2022,kulikuwa na matukio 12,163 ya ukatili ambapo ubakaji ni 6,335,ulawiti ni 1,557 na mimba za utotoni ni 1,555 kwa mujibu wa jeshi la polisi. Akizungumza jijini Dar es salaam Julai 17,2023 katika mkutano wa viongozi wa dini na Serikali,Jingu amesema hadi kufikia machi,2023 watoto wanaoitwa wa mitaani walikuwa 335,971,kati Yao wakiume 168,634 na wakike 167,337 na walibainishwa kuishi katika Mazingira hatarishi. "Jumla ya watoto 2,185 kati Yao wa kiume 1,324 na wakike 861 walikuwa wanafanya kazi na kuishi Mitaa ,baadhi Yao waliunganishwa na familia zao Serikali imeratibu uanzishwaji wa makao ya watoto 333 ya Serikali na binafsi ambayo yanahifadhi watoto 12,077 Ameongeza kuwa kwa Sasa

KATIBU TAWALA AFANYA ZIARA WILAYA YA KALAMBO

Image
 Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Bw.Gerald Kusaya amefanya ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya Kalambo. Lengo la Ziara hiyo ni kukagua miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa Wilayani humo.Mradi aliyotembelea ni ujenzi wa Soko la kisasa la samaki utakaogharimu Tshs.Bilion 1.5 mpaka kukamilika kwake. Ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kwa usimamizi mzuri wa ujenzi huo unaofanyika katika kata ya Kasanga. Akizungumza katika eneo la mradi Katibu Tawala wa Mkoa ameeleza kuwa ujenzi wa Soko Hilo utasaidia wavuvi wanaoendesha shughuli zao katika ziwa Tanganyika kupata uhakika wa Soko la samaki,Hali itakayosaidia kuinua uchumi wa wavuvi hao na kuchangia ongezeko la makusanyo ya Mapato kwa Halmashauri ya Wilaya Kalambo. Miradi mingine iliyokaguliwa ni pamoja na ujenzi wa shule mpya ya msingi Matai 'B' kupitia mradi wa BOOST,ujenzi wa madarasa mawili ya awali shule ya msingi kilewani kupitia mradi wa BOOST na ujenzi wa madarasa mawili shule ya msingi Kilewani kupitia

POLISI YAZUIA CCM KUANDAMANA

Image
 Jeshi la polisi Tanzania limepiga marufuku maandamano yaliyoitishwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) katika Wilaya zote Tanzania ili kuunga mkono Serikali juu ya Uwekezaji katika bandari. Msemaji wa polisi,David Misime amesema"July 16,2023 kupitia Vyombo vya Habari mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii ameonekana Mwenyekiti wa UVCCM akitoa taarifa ya kuhamasisha maandamano katika Wilaya zote na wataanza na Dar es salaam July 18,2023 ili kuiunga mkono Serikali juu ya Uwekezaji katika bandari,Sheria ipo wazi kwa mtu au kikundi Cha watu kinapotaka kuishi maandamano taratibu zipi zinatakiwa kufuatwa". "Pamoja na utaratibu huo wa kisheria,kuitisha maandamano Nchi nzima ni sawa na kutaka kuleta vurugu na hofu kwa watanzania bila sababu yoyote Ile kwani yapo majukwaa ya kuwasilisha jambo lolote lililo katika utaratibu wa kisheria bila kuhamasisha maandamano ya aina hiyo". Kwa msingi huo, Jeshi la polisi linapiga marufuku maandamano hayo yasifanyike na hii ni

USALAMA WA MWANDISHI KAZINI UZINGATIWE,WAPO HATARINI.

Image
 Mkurugenzi wa Klabu za Muungano wa waandishi wa Habari Nchini (UTPC)Bw.Kenneth Simbaya amewataka Waandishi wa Habari kutosita kutoa taarifa katika Klabu za Waandishi wa Habari zilizopo mikoani mwao wanapofanyiwa vitendo vya udhalilishaji au kutishiwa usalama wao na wadau. Simbaya ameyasema hayo wakati akiongea na uongozi na wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Kigoma (KGPC) ikiwa ni ziara yake maalumu kujitambulisha Kwa wanachama lakini pia kueleza namna ya ufanisi katika mpango wa move From Good to Great unaolenga mabadiliko Chanya ya press clubs Nchini. Amesema zipo taarifa za Waandishi wengi kufanyiwa madhila na wadau ikiwemo kushushwa njiani katika ziara,vitisho,ubaguzi na unyanyapaa mambo ambayo yanakwamisha ufanisi wa Mwandishi kuripoti Habari kwa maslahi ya umma.

Halmashauri Ya Kalambo Yafanikiwa Kupunguza Utapiamlo Kwa Watoto Chini Ya Miaka 5

Image
  Halmashauri ya Kalambo mkoani Rukwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 imefanikiwa kutekeleza mpango kabambe wa lishe wa taifa kwa kupunguza utapiamlo mkali kwa watoto chini ya miaka mitano. Utekelezaji wa mpango huo umekuwa ukitekelezwa na idara ya afya kwa kushirikina na idara mtambuka ambazo ni kilimo, elimu msingi na elimu sekondari kwa kutoa elimu ya lishe bora katika jamii kupitia vituo vya kutolea huduma za afya ikiwemo ulaji wa vyakula vyenye virutubishi. Mapema akiongea kupitia kikao cha kamati ya lishe ya wilaya kilicho fanyika katika ukumbi wa mkuu wa wilaya hiyo Robert Tepeli, alisema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 Halmashauri ilifanikiwa kukagua vyakula na madini joto ikiwemo chumvi zinazo uzwa madukani sambamba na unyweshaji Vitamin (A) na kutoa dawa za minyoo kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya. Alisema katia kipindi hicho walifanikiwa kutekeleza zoezi la utoaji elimu kwa watoa huduma za Afya juu ya utambuzi wa utapiamlo na matibabu kulingana n

WANANCHI NSIMBO WAMPONGEZA MBUNGE NA MKURUGENZI UJENZI WA SHULE

Image
 NA George Mwigulu.Nsimbo. Wananchi wa kitongoji Cha Songambele Kijiji Cha Tumaini kata ya Itenka Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi wamekiri kuwa matatizo ya utoro shuleni na mimba za utotoni zitakoma baada ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa shule ya msingi Makomelo. Ujenzi wa shule hiyo unatekelezwa chini ya mradi wa Boost ambapo fedha Mil 561 zinatumika kwenye ujenzi wa vyumba vya madarasa 16 sambamba na vifaa vya samani kama vile madawati. Masolwa Malubano,Mkazi wa kitongoji Cha Songambele ameeleza wamekuwa na matatizo ya watoto wao kwenda shule umbali zaidi wa kilometa tisa(9) jambo ambalo licha ya juhudi kubwa za kuchangia chakula mahala pakusomea lakini Bado watoto wao walishindwa kumudu umbali.

MJADALA WA DP WORLD WAIBUKIA RUKWA MBUNGE VITI MAALUMU ANENA

Image
 Na Israel Mwaisaka. Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Rukwa Bupe Mwakang'ata(CCM)amewaondoa hofu wananchi juu ya Uwekezaji bandarini unaofanywa na Serikali na kuwapuuzia wale wote wanaokashifu Uwekezaji huo kupitia DP WORLD. Akizungumza kwenye kikao Cha Baraza la wanawake UWT wilayani Nkasi amesema kuwa kuwepo na maneno mengi ya upotoshaji juu ya Uwekezaji unaofanywa na Serikali katika kuboresha shughuli za bandari Nchini na kuwa  lengo ni kutaka kukuza Mapato yatokanayo na bandari ili kipato kinachopatikana kiweze kutoa huduma kwa jamii. Amesema ni muda mrefu Serikali imekuwa ikitafuta namna nzuri ya kuleta Tija katika bandari zetu Nchini na Moja ya njia hizo ni za Uwekezaji na Sasa wamejiyokeza watu ambao wanaupinga bila sababu za msingi na kutaka waende wakawe mabalozi wazuri na kuelekeza Nia njema ya Serikali juu ya Uwekezaji ambao Sasa DP WORLD wameonesha Nia ya kuwekeza katika eneo Hilo la bandari.

MBUNGE LUPEMBE APANIA KUWA NA TIMU ITAKAYOSHIRIKI LIGI YA NBC.

Image
 Na.George Mwigulu Wachezaji arobaini(40)wa mpira wa miguu katika Jimbo la Nsimbo wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi watachaguliwa wakati wa ligi ya Jimbo (LUPEMBE CUP)kwa ajili ya kuingia Kambi ya kuendeleza vipaji na kutengeneza timu itakayowezesha mbio za kushiriki ligi kuu Tanzania Bara(NBC). Kwa miaka mingi mkoa wa Katavi licha ya juhudi mbalimbali kufanywa na viongozi na wadau wa michezo lakini umekosa timu hata Moja inayoshiriki kwenye mashindano mbalimbali hususani NBC. Akizungumza kwenye mkutano katika Kijiji Cha Tumaini kata ya Itenka Halmashauri ya Wilaya Nsimbo mkoa wa Katavi,Mbunge wa Jimbo la Nsimbo,Anna Lupembe ameeleza kuwa lengo kubwa kwenye mashindano ambayo amekuwa akiyafadhili ni kuibua vipaji kwa vijana hasa kupitia michezo kama inavyoelekezwa kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM). Lupembe ameeleza kwa muda mrefu amekuwa akifadhili mchezo wa mpira wa miguu katika Jimbo lake kupitia ligi ya Lupembe CUP ambayo amebaini Kuna vijana wengi wanavipaji vikubwa hivyo hawez

Watoto 80,486 Kufikiwa Na Kamapeni Ya Chanjo Ya Polio Wilayani Kalambo

Image
 Na Baraka Lusajo - Rukwa  Ofisi ya Rais TAMISEM kwa kushirikina na wizara ya afya imepanga kuendesha kamapeni ya polio kwa mikoa minne inayopakana na nchi za Zambia ikiwemo mkoa wa Rukwa,katavi , Songwe   na Mbeya ili kuwakinga watoto chini ya miaka 5 dhidi ya ugonjwa huo. Hayo yamebainishwa na kaimu mganga mkuu wa Halmashauri ya Kalambo Dr.Emmanuel Kisyombe kupitia kikao cha kamati ya afya ya msingi ( PHC) kilicho fanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo June 6/2023,Ambapo amesema kampeni hiyo inarajiwa kuanza Julai 27/2023 na kuhitimishwa Julai 30/2023. ‘’Chanjo ambayo itatumika katika kampeni hii ni chanjo ya polio ya sindano (IPV) ambayo ina mpa kinga mtoto dhidi ya polio virus type 2’’na kwamba zaidi ya watoto 80,486 wanatarajiwa kufikiwa kupitia kampeni hiyo’’ alisema Dr Kisyombe. Mapema akiongea kupitia kikao hicho mkuu wa wilaya hiyo Lazaro Komba aliwataka wataalamu wa afya wilayani humo kuendelea kushirikina na wadau wakiwemo viongozi wa dini katika kudhibiti ugonjwa

Dc Kalambo Ataka Walio Husika Kumuozesha Mwanafunzi Wa Darasa La Saba Kukamatwa

Image
Mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Lazaro Komba ameliagiza Jeshi la polisi wilayani humo kuwakamata wazazi na walezi waliomwozesha mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Mbuza kata ya Mkowe mwenye umri wa miaka 17 na kumuozesha kwa Asulwa Sikombe mkazi wa kijiji cha Mbuza. Taarifa kutoka kwa kwenye uongozi wa kijiji hicho akiwemo mwenyekiti wa kijiji hicho Alisen Machenchelwa na mkuu wa shule hiyo Fedelisi Mbuluko zimeeleza kuwa mwanafunzi huyo Mach 2023 alitoroka kwenye makazi ya wazazi wake na kutokomea kusiko fahamika na kwamba baada ya kurejea June 2023 wazazi wake walimua kumuozesha kwa ndugu Asulwa Sikombe mkazi wa kijiji cha Mbuza. Walieleza kuwa baada ya kupata taarifa hizo waliamua kuwakamata wazazi wa binti huyo na kuwafikisha kwenye kituo cha polisi Matai kwa hatua zaidi. Hata hivyo mapema akiongea ofisini kwake mkuu wa wilaya hiyo Lazaro Komba amesema mpaka sasa Jeshi la polisi linamsaka aliyeozeshwa mwanafunzi huyo na kwamba wazazi wawili wa mwanafun