MBUNGE WA JIMBO LA KWELA NA MKURUGENZI MANISPAA YA SUMBAWANGA WAONGOZA HARAMBEE UJENZI WA KANISA KATILIKI.

 Mbunge wa Jimbo la Kwela Mheshimiwa Deus Clement Sangu na Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Bi.Catherine Mashallah wameongoza harambee ya ujenzi wa kanisa la parokia ya Mt.Fransisco wa Asiz Jimbo la Sumbawanga.


Mbunge wa Jimbo la Kwela Mh.Sangu ametoa kiasi Cha shilingi Milioni tatu  ajili ya ujenzi wa kanisa la parokia hiyo.

Mh.Sangu amesema,"Kwa namna nilivyoona parokia hii mnavyojitoa nimefarijika sana mimi kama Mwanaparokia nimewiwa sana naamini MwenyeziMungu ataniwezesha Kila wakati  kuweza kupata nguvu yakuja  kujenga kanisa hili kwa pamoja"


Nae Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Bi.Catherine Mashalla amechangia mifuko mia Moja (100) ya saruji katika ujenzi wa kanisa Hilo wakati wa uendeshaji wa harambee ya ujenzi huo,nakuwaambia waumini wa parokia hiyo kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan inafanya Kazi kubwa hivyo ni jukumu letu kuunga mkono mambo yote anayoleta Rais wetu kwa kuyasimamia,kuyatunza na kuyalinda.


 Aidha,akitoa salamu za shukrani Paroko wa parokia hiyo ya Mtakatifu Fransisco wa Asiz Padri Didas Issacus Nandi ameipongeza Serikali kwa kuendeleza amani,Umoja na Mshikamano na Taasisi za kidini.Pia Serikali kutoa ushirikiano katika sekta mbalimbali bila kujali dini yoyote na kutufanya wote kuwa kitu kimoja.




Comments

Popular posts from this blog

Wakulima Rukwa kutumia zana bora kuongeza uzalishaji wa mazao msimu mpya wa kilimo

UTPC KUENDELEA KUELIMISHA UMMA,UMUHIMU WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

MAENDELEO YA CHUO CHA UALIMU SUMBAWANGA