USALAMA WA MWANDISHI KAZINI UZINGATIWE,WAPO HATARINI.

 Mkurugenzi wa Klabu za Muungano wa waandishi wa Habari Nchini (UTPC)Bw.Kenneth Simbaya amewataka Waandishi wa Habari kutosita kutoa taarifa katika Klabu za Waandishi wa Habari zilizopo mikoani mwao wanapofanyiwa vitendo vya udhalilishaji au kutishiwa usalama wao na wadau.




Simbaya ameyasema hayo wakati akiongea na uongozi na wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Kigoma (KGPC) ikiwa ni ziara yake maalumu kujitambulisha Kwa wanachama lakini pia kueleza namna ya ufanisi katika mpango wa move From Good to Great unaolenga mabadiliko Chanya ya press clubs Nchini.


Amesema zipo taarifa za Waandishi wengi kufanyiwa madhila na wadau ikiwemo kushushwa njiani katika ziara,vitisho,ubaguzi na unyanyapaa mambo ambayo yanakwamisha ufanisi wa Mwandishi kuripoti Habari kwa maslahi ya umma.



Comments

Popular posts from this blog

WALIOFUKUA KABURI WAKAMATWA NA JESHI LA POLISI RUKWA

Wakulima Rukwa kutumia zana bora kuongeza uzalishaji wa mazao msimu mpya wa kilimo

ZIMAMOTO YATOA MAFUNZO KWA WATUMISHI RUKWA.