POLISI YAZUIA CCM KUANDAMANA

 Jeshi la polisi Tanzania limepiga marufuku maandamano yaliyoitishwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) katika Wilaya zote Tanzania ili kuunga mkono Serikali juu ya Uwekezaji katika bandari.

Msemaji wa polisi,David Misime amesema"July 16,2023 kupitia Vyombo vya Habari mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii ameonekana Mwenyekiti wa UVCCM akitoa taarifa ya kuhamasisha maandamano katika Wilaya zote na wataanza na Dar es salaam July 18,2023 ili kuiunga mkono Serikali juu ya Uwekezaji katika bandari,Sheria ipo wazi kwa mtu au kikundi Cha watu kinapotaka kuishi maandamano taratibu zipi zinatakiwa kufuatwa".


"Pamoja na utaratibu huo wa kisheria,kuitisha maandamano Nchi nzima ni sawa na kutaka kuleta vurugu na hofu kwa watanzania bila sababu yoyote Ile kwani yapo majukwaa ya kuwasilisha jambo lolote lililo katika utaratibu wa kisheria bila kuhamasisha maandamano ya aina hiyo".

Kwa msingi huo, Jeshi la polisi linapiga marufuku maandamano hayo yasifanyike na hii ni pamoja na watu wengine pia wenye Nia kama hizo na badala yake wawasilishe hoja zao kupitia Mikutano na Vyombo vya Habari.

Comments

Popular posts from this blog

Wakulima Rukwa kutumia zana bora kuongeza uzalishaji wa mazao msimu mpya wa kilimo

UTPC KUENDELEA KUELIMISHA UMMA,UMUHIMU WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

MAENDELEO YA CHUO CHA UALIMU SUMBAWANGA