HALMASHAURI ZAAGIZWA KUSIMAMIA KUSIMAMIA MIRADI YA BOOST.
Mkurugenzi TAMISEMI anayeshughulikia masuala ya Elimu Vicent Kayombo amemtaka Maafisa Elimu kwenye Halmashauri zote mkoani Rukwa kusimamia kwa ukaribu ujenzi wa miradi ya madarasa yanayojengwa maarufu kama miradi ya BOOST.
Akizungumza na Maafisa Elimu wa ngazi zote mkoani Rukwa Mkurugenzi huyo wa TAMISEMI alisema hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa miradi hiyo ambayo imekuwa ikitekelezwa pasipo kwenda na wakati.
Kayombo ametoa agizo Hilo baada ya kufanya ukaguzi wa baadhi ya majengo na kutoridhishwa na kasi yake ya ujenzi wake.
Hata hivyo licha ya kusisitiza Maafisa Elimu kusimamia majengo hayo ya Boost aliwataka kusimamia huduma Bora kwa walimu kwenye maeneo Yao ya kazi sanjari na kuwasikiliza hoja zao na kuzitafutia ufumbuzi yakiwapo madai Yao na upandaji wa madaraja.
Aidha aliwapongeza watendaji wa idara ya Elimu kwa kufanikisha ufaulu mzuri wa wanafunzi katika matokeo ya kidato Cha sita kwa asilimia 99 na kufuta Zero katika mwaka 2023.
Comments
Post a Comment