Posts

Showing posts from September, 2021

NFRA YANUNUA TANI 4,600 ZA MAHINDI YA WAKULIMA RUKWA

Image
  Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA) imefanikiwa kununua tani 4,600 za mahindi zenye thamani ya Shilingi Bilioni Mbili na Milioni Mia tatu ( 2,300,000,000) toka kwa wakulima kati ya lengo la tani 5,000 zilizopangwa awamu ya kwanza kufikia Agosti 31, mwaka huu. Hayo yamebainishwa leo (01.09.2021) wakati Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Milton Lupa alipokutana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti ofisini kwake Sumbawanga akiwa katika ziara ya kukagua zoezi la ununuzi wa mahindi Meupe linaloendelea katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

RC MKIRIKITI: TRA SIMAMIENI SHERIA ZA KODI

Image
 Mkuu wa mkoa wa Rukwa MH.JOSEPH MKIRIKITI amewataka TRA Mkoa wa Rukwa kuhakikisha wanasimamia sheria za kodi,kutoa elimu ili ukusanyaji kodi katika mkoa wa Rukwa uweze kuleta maendeleo ''SIMAMIENI SHERIA MAHAKAMA ZIPO ZITASHUGULIKA SIO KILA KITU KIZURI DAR ES SALAAM TUTUMIE MAPATO YETU KUBORESHA MAENEO YETU'' Amesema hayo katika kikao cha kamati ya kusimamia,kudhibiti na kuratibu mapato na matumizi ya serikali.Imenadaliwa na Peter Helatano

WEKENI MKIKAKATI KUPUNGUZA TATIZO HILI

Image
  Mkuu wa wilaya sumbawanga Mh.Sebastian Warioba amewaagiza madiwani kuhakikisha wanatafuta namna nzuri ya kudhibiti wimbi la watoto wa mitaani katika maeneo yao,Ametoa agizo hilo katika balaza la madiwani lilifanyika katika ukumbi wa manispaa ya Sumbawanga ..’Watoto ni wengi na wanaongezeka hivyo tuwe na mikakatati ya kushirikisha wadau kama NGOs na wadau wengine kuwachukua watoto hao na kuwapatia elimu kwani wengine ni wadogo kabisa umri wa kwenda shule. Watoto hawa watakuja kuwa hatari sana tusipokuwa makini.imeandaliwa na PETER HELATANO