MJADALA WA DP WORLD WAIBUKIA RUKWA MBUNGE VITI MAALUMU ANENA
Na Israel Mwaisaka.
Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Rukwa Bupe Mwakang'ata(CCM)amewaondoa hofu wananchi juu ya Uwekezaji bandarini unaofanywa na Serikali na kuwapuuzia wale wote wanaokashifu Uwekezaji huo kupitia DP WORLD.
Akizungumza kwenye kikao Cha Baraza la wanawake UWT wilayani Nkasi amesema kuwa kuwepo na maneno mengi ya upotoshaji juu ya Uwekezaji unaofanywa na Serikali katika kuboresha shughuli za bandari Nchini na kuwa lengo ni kutaka kukuza Mapato yatokanayo na bandari ili kipato kinachopatikana kiweze kutoa huduma kwa jamii.
Amesema ni muda mrefu Serikali imekuwa ikitafuta namna nzuri ya kuleta Tija katika bandari zetu Nchini na Moja ya njia hizo ni za Uwekezaji na Sasa wamejiyokeza watu ambao wanaupinga bila sababu za msingi na kutaka waende wakawe mabalozi wazuri na kuelekeza Nia njema ya Serikali juu ya Uwekezaji ambao Sasa DP WORLD wameonesha Nia ya kuwekeza katika eneo Hilo la bandari.
Comments
Post a Comment