MBUNGE LUPEMBE APANIA KUWA NA TIMU ITAKAYOSHIRIKI LIGI YA NBC.

 Na.George Mwigulu

Wachezaji arobaini(40)wa mpira wa miguu katika Jimbo la Nsimbo wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi watachaguliwa wakati wa ligi ya Jimbo (LUPEMBE CUP)kwa ajili ya kuingia Kambi ya kuendeleza vipaji na kutengeneza timu itakayowezesha mbio za kushiriki ligi kuu Tanzania Bara(NBC).



Kwa miaka mingi mkoa wa Katavi licha ya juhudi mbalimbali kufanywa na viongozi na wadau wa michezo lakini umekosa timu hata Moja inayoshiriki kwenye mashindano mbalimbali hususani NBC.

Akizungumza kwenye mkutano katika Kijiji Cha Tumaini kata ya Itenka Halmashauri ya Wilaya Nsimbo mkoa wa Katavi,Mbunge wa Jimbo la Nsimbo,Anna Lupembe ameeleza kuwa lengo kubwa kwenye mashindano ambayo amekuwa akiyafadhili ni kuibua vipaji kwa vijana hasa kupitia michezo kama inavyoelekezwa kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM).

Imeshindwa kupakia ''. Invalid response: RpcError

Lupembe ameeleza kwa muda mrefu amekuwa akifadhili mchezo wa mpira wa miguu katika Jimbo lake kupitia ligi ya Lupembe CUP ambayo amebaini Kuna vijana wengi wanavipaji vikubwa hivyo hawezi kuviacha pekee yake kwenye hatua ya chini na kupotea.





















Comments

Popular posts from this blog

Wakulima Rukwa kutumia zana bora kuongeza uzalishaji wa mazao msimu mpya wa kilimo

UTPC KUENDELEA KUELIMISHA UMMA,UMUHIMU WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

MAENDELEO YA CHUO CHA UALIMU SUMBAWANGA