Posts

Showing posts from September, 2020

Ahukumiwa Mwaka Mmoja Na Nusu Kwa Kosa La Wizi

Image
  Na baraka  Lusajo  - Rukwa Mahakama ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa imemuhukumu kwenda jela mwaka mmoja na nusu Frank Geoffrey Sikazwe (28) mkazi wa kijiji cha Kasanga wilayani humo kwa kosa la wizi. Mtuhumiwa alishitakiwa kwa makosa mawili baada ya   kuvunja nyumba ya Lauriano Simbeye huko Kasanga usiku wa tarehe 05 Februari 2020, akiwa na kusudio la kuiba kinyume na kifungu 294(1)(a) and (2) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya mwaka 2019, pia kosa la wizi kinyume na kifungu 258(1)(2)(a) na 265 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya mwaka 2019. Mtuhumiwa alikamatwa na kufikishwa kituo cha polisi Matai na kuandaliwa hati ya mashitaka hatimaye kufikishwa mahakamani. Baada ya kusomewa mashitaka alikana kutenda kosa hilo suala lililopelekea upande wa mashitaka kuwa na jukumu la kuthibitisha pasi na shaka tuhuma zinazomkabili mshitakiwa.   Upande wa mashitaka ukiongozwa na mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi Mrisho Kimbeho ulitafuta mashahidi ndi

Bongo Movie na Bongo Fleva wakutanishwa kwenye Michezo kuamua mbabe.

Image
 Na Baraka Lusajo. Rukwa Katika kuendeleza na kukuza amani, upendo, mshikamano na kudumisha umoja kwa wasanii wanaoigiza maarufu kama “Bongo Movie” pamoja na wasanii waimbaji maarufu kama “Bongo Fleva”, Afisa Utamaduni wa Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa Kiheka Charles amezikutanisha timu za makundi hayo mawili katika mechi ya mpira wa miguu iliyopigwa katika viwanja vya shule ya sekondari Mazwi mjini Sumbawanga. “Michezo ni Afya, Sanaa ina kazi ya kuelimisha na kuburudisha, sanaa huifanya jamii kuwa kitu kimoja, na michezo pia huifanya jamii kuwa kitu kimoja na tunashirikiana katika mambo mbalimbali hasa katika kutangaza kampeni zetu mbalimbali za kimaendeleo, kutangaza fursa zinazopatikana ndani ya manispaa yetu ya Sumbawanga na tukifanya vizuri, unajua ile sumbawanga iliyokuwa inasifika zamani ile sifa itapotea, nadhani wenye mnaona watu wakija kutoka mbali wanaona tofauti na walivyokuwa wanafikiria,” Alisema  Kiheka. Kwa upande wao washiriki wa mchezo huo waliishukuru Ofisi

Wakulima Rukwa kutumia zana bora kuongeza uzalishaji wa mazao msimu mpya wa kilimo

Image
Na  Baraka Lusajo - Rukwa. Vyama vya Ushirika wilayani Kalambo mkoani Rukwa vimetakiwa kuwekeza nguvu zao katika upatikanaji wa zana bora za kilimo ili kuweza kuongeza uzalishaji na ubora wa mazao mbalimbali mkoani Rukwa hasa katika kipindi hiki wanachojiandaa kuanza msimu mpya wa kilimo unaotarajiwa kuanza mwezi Oktoba mwaka huu.   Akiongea wakati wa Ufunguzi wa uzinduzi wa Mkakati wa matumizi bora ya zana za kilimo, Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Rukwa, Ocran Chengula alisema kuwa, asilimia 80 ya uchumi wa Mkoa wa Rukwa unategemea kilimo lakini ni asilimia 3 tu ya wakulima wanatumia matrekta hali inayopekelea eneo kubwa la ardhi inayofaa kulimwa katika mkoa huo kutolimwa na pia kutopata mazao bora yenye kuhimili ushindani katika soko la dunia. “Katika mkoa wetu kuna hekta 1,660,000 ambazo zinafaa kwa kilimo, lakini kati ya hizo kwa kiasi kikubwa sana tunazoloma ni hekta laki tano na kidogo, ambazo ni sawa na asilimia 32 kuna kipindi tulif