WATOTO WATATU FAMILIA MOJA WAFA MAJI WAKIVUA SAMAKI KATAVI
Na.Mary Clemence,Katavi
Watoto watatu wa familia Lucia Kazima(10),Kabisi Lazima(8),na Makala Lazima(6) wakati wa kitongoji Cha Kayenze B Wilayani Mpanda wamekufa Maji wakati wakivua samaki katika mto Kamilala.
Watoto hao walikuwa wanafunzi wa shule ya msingi Kamilala ambapo Lucia alikuwa akisoma darasa la 5,Kabisi darasa la nne na Makala darasa la kwanza.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Katavi,Kaster Ngonyani akizungumza na Waandishi wa Habari Leo jumatano Julai 19,2023 amesema tukio Hilo limetokea Julai 13,2023 saa 7:45 mchana.
"Eneo la mto huo linatumika pia kwa shughuli za uvuvi samaki,watoto hao walikwenda kuvua samaki,haikufahamika kama walikuwa wanaogelea au ilikuwaje,"amesema.
"Kwa sababu hii miili Yao ilikutwa ikielea na wasamalia wema walitoa taarifa polisi Kisha iliopolewa na kufanyiwa Uchunguzi Kisha ndugu wakakabidhiwa kwa ajili ya taratibu za maziko,"amesema Kaster.
Kamanda Ngonyani ametoa Rai kwa wazazi na walezi kuwa na uangalizi wa karibu pindi watoto wao wanapotoka nyumbani kwenda kujitafutia kipato.
Comments
Post a Comment