Posts

Showing posts from December, 2022

MKUTANO MAALUM WA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI RUKWA

Image
 PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA MKUTANO MAALUM WA KLABU YA WANDISHI WA HABARI MKOA WA RUKWA

SERIKALI KUWEKA MIPAKA KULINDA VYANZO VYA MAJI

Image
  SERIKALI KUWEKA MIPAKA KULINDA VYANZO VYA MAJI Serikali Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa imeanza Uwekaji wa mipaka kati ya Pori la Akiba Lwafi na Kijiji cha Mtogolo kilichopo Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa ili Kulinda chanzo cha maji katika bwawa la Mfili amabalo ni tegemeo la maji Katika Wilaya ya Nkasi kutokana na bwawa hilo kukausha maji kutokana na shuguli za kibinadamu zinazodaiwa kufanyika pembezoni mwa bwawa hilo. Hayo yamejiri Katika zoezi la uhuishaji wa   hifadhi ya msitu wa Lwafi ambopo Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Peter Lijualikali amewataka wananchi kuzingatia maelekezo ya Serikali ili kulinda vyanzo vya maji Wananchi Katika maeneo hayo wanadai kuishi mda mrefu huku kilio chao ni kuhakikisha wanapatiwa maeneo mengine kama walivyoahidiwa na Serikali

WANANCHI WAOMBA ULINZI WA JESHI MWAMBAO MWA ZIWA TANGANYIKA.

Image
  WANANCHI WAOMBA ULINZI WA JESHI MWAMBAO MWA ZIWA TANGANYIKA. Na Peter Helatano Wakazi wa Vijiji vya Kata za KIZUMBI, WAMPEMBE, KIRANDO, na KABWE Katika wilaya ya NKANSI, Mkoani Rukwa, wameiomba Serikali Ulinzi kutokana na wimbi la Ujambazi kukithiri mwambao mwa ziwa Tanganyika upande wa Vijiji hivyo. Katika Mkutano wa hadhara uliofanhyika katika Kijiji cha LYAPINDA, Kata ya KIZUMBI, wananchi wamemwambia Mkuu wa mkoa kuwa watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wamekuwa wakipora Mali na   vifaa vyao vya Uvuvi, na kusababisha hofu kwa wananchi wa vijiji kuzunguka ziwa Tanganyika upande wa mkoa wa Rukwa. Katika mkutano wa hadhara wa wananchi wa Vijiji vya Kata ya Kizumbi na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa QUEEN SENDIGA. Mkutano huo wa wananchi umelenga kueleza kero zao zinazowakabili za kukosekana kwa usalama mwambao mwa ziwa Tanganyika. Wananchi wakaenda mbali zaidi kuomba kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzani-JWTZ ili kukomesha matukio ya ujambazi.   Mkuu wa Mkoa wa Rukwa QUEEN SENDIGA