Posts

Showing posts from November, 2021

MUNGU AMEKUCHAGUA HATUNA BUDI KUMUOMBA

Image
  Na Franco NKYANDWALE Sumbawanga 1. Frola (1966-2021 ) umejitenga kimapenzi na Nswima, Mungu amekuchagua. 2. Hakufanya kwa hiyari, bali kama ua ulichanua na sasa limefunga kabisa. 3. Jicho la Nswima lina chozi chepechepe wa kufuta hakuna, ila MAULANA mfariji. 4. Naandika nikitetema leo yako Frola, umetangulia mbele ya haki, baadaye yetu zamu tutaonana. 5. Ndoa mliifunga, sasa kifo kimetengua Nswima moyoni amepwaya na kuwaya waya. 6. Frola bado jamii inakuhitaji mola kasema basi, Mungu amjazi faraja Nswima na familia. 7. Kila kona ni kilio hata kule Karema watu walia upweke umetuachia wategemezi ni machozi,TANZANIA yalia. 8. Mengi ulitenda kwa wema na faraja, leo tumejawa na simanzi, yako umemaliza ukurasa umefunga Frola. 9. Hakuna wa kutangua kifo hicho, kwa sote hatukwepi mioyo yetu imekinunia kifo, lakini hakuna namna. 10. Kwa mola utangulie, nawe ujuwe kwetu ni majonzi kwa Nswima ni zaidi. BURIANI Frola.  11. Majukumu na upweke Frola umemwachia Nswima, nafsini hatakusahau kamwe, Ja

RED CROSS WATAKIWA KUANDAA MAFUNZO YA UOKOAJI MASHULENI

Image
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa  Joseph  Mkirikiti leo amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Chama cha Red Cross Mkoa wa Rukwa  ambapo amewataka waandae programu ya maokozi kwenye shule za Rukwa ili vijana wengi wawe na umahili wa kuokoa jamii pale majanga yanapotokea. Mkirikiti amesema hayo leo ofisini kwake mjini Sumbawanga pia ameupongeza uongozi wa Red Cross kwa kazi wanayoendelea kuifanya kwenye jamii ya Rukwa huku akiwataka wawe na ushirikiano na Skauti pamoja na Jeshi la Zimamoto. "Hamasisheni kampeni ya Damu Salama kwenye mkoa wetu mkishirikiana na Hospitali zetu za Halmashauri hususan maeneo ya vijijini hatua itakayosaidia kuokoa maisha ya watu " alisema Mkirikiti  Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti  wa Red Cross Rukwa Saada Kimanta ameomba ushirikiano na uongozi wa mkoa ili watambulike na kupewa kipaumbele kwenye utekelezaji wa malengo ya Red Cross. Aliongeza kusema Red Cross tunahitaji kushirikishwa kwenye shughuli za mkoa na kitaifa ikiwemo ziara za viongozi wa kita

DAVIDO AFANYA USAMARIA WEMA

Image
Na Peter Helatano..0621374025  Msanii maarufu nchini Nigeria DAVIDO aliendesha kampeni kupitia mtandao wa kijamii Instagram akiwaomba marafiki zake mbalimbali Afrika wanamziki akiwemo Diamond Platnumz kumchangia fedha kwa ajili ya Maandalizi ya Siku yake ya Kuzaliwa.. Birthday..Baada ya kufanikisha Jambo hilo kwa kuchangiwa kiasi Cha Bilioni 2.5 Fedha hizo hatimaye Amezieleka kwa Watoto yatima kuwapatia msaada.Hili no funzo pia kwa wasanii wengine wakubwa wanapofanya Anasa wasiwasahau watu wenye Mahitaji,Kwani Hali hiyo itakufanya kuwa na Baraka Katika shuguli zako.Jiulize wewe umewahi kufanya Nini amabacho unahisi ni moja ya Sadaka Katika maisha yako.

DKT.MOLLEL AHIMIZA KUWASAIDIA WANANCHI WENYE MAHITAJI

Image
 Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel ameuagiza uongozi wa Afya Mkoa wa Tanga chini ya Mganga Mkuu wa Mkoa huo kuhakikisha Kijana Elias Mgomela (27) mkazi wa Jijini Tanga kupelekwa haraka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufanyiwa upasuaji wa uvimbe alionao shavuni. Elias amekuwa akiishi na uvimbe huo toka mwaka 2007 baada ya kukosa fedha za matibabu na amekuwa akifanya shughuli za kuimba na kucheza katika vikundi vya ngoma vya uelimishaji na uburudishaji jamii ndani ya Jiji la Tanga. Dkt. Mollel ameihimza jamii kuendelea kusaidia wananchi wenye mahitaji ya kupata tiba kama wanavyochangia kwenye shughuli nyinginezo kama vile harusi na misiba.

MWONGOZO WA KUPAMBANA NA RUSHWA KWA VIJANA WA SKAUTI RUKWA

Image
  MWONGOZO WA KUPAMBANA NA RUSHWA KWA VIJANA WA SKAUTI RUKWA  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Joseph Mkirikiti leo amekabidhiwa mwongozo wa kupambana na rushwa kwa vijana wa skauti mkoa wa Rukwa kwenye hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Sumbawanga.  Akikabidhi Mwongozo huo ,Kamanda wa TAKUKURU  Mkoa wa Rukwa Bw. Daniel  Ntera  alisema lengo la serikali ni kuona vijana wakifundishwa njia mbalimbali za kukabiliana na rushwa wakiwa mashuleni.  Mwongozo huo utatumika kwa vijana wa skauti kuanzia shule za msingi, sekondari hadi vyuo ambapo pia walimu watatumika kufundishia elimu ya kudhibiti na kupambana na rushwa kwenye jamii ya watanzania.

Visit Kalambo water falls

Image
 Na Peter Helatano Visit to Kalambo water falls...Tembelea Mapolomoko ya maji Kalambo Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Tano Mwera amesema maandalizi kwa ajili ya ziara ya kutembelea kivutio cha utalii cha maporomoko ya maji ya Kalambo yamekamilika na kuwa sasa yatafanyika tarehe 18 Desemba mwaka huu lengo ikiwa kukuza utalii wa ndani ya Mkoa wa Rukwa . Mwera ametoa taarifa hiyo leo mjini Sumbawanga alipoongea na wanahabari.Ikumbukwe Kalambo water Falls Ni Mapolomoko ya Pili kwa ukubwa kutoka Yale ya Afrika kusini.Pia ina vivutio vya misitu ya Asili,Hifadhi na Maeneo ambayo yanavutia kiutalii.Yapo maeneo ya kuweka makambi kwa ajili ya kuchoma Nyama,ngoma,Kuogelea, Jogging na Burudani mbalimbali huku ukilitazama jua la kuzama kwa uzuri(Sun set) kupitia ziwa Tanganyika,ziwa lililojaa Samaki wenye Radha ya kipekee barani Afrika.Maji yake meupe yenye kukuwezesha kuona kina kwa chini na kukupa urahisi Kuogelea.Tembelea maeneo hayo usiishie tu kusimuliwa.

SKAUTI KUANZA KUFANYA KAZI YA KUPAMBANA NA RUSHWA RASMI

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Joseph Mkirikiti akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa Mafunzo kwa Vijana wa Skauti kuhusu Kuzuia na Kupambana na Rushwa ambapo leo ametoa wito kwa Maafisa Elimu kutumia mwongozo huo kudhibiti vitendo vya wanafunzi wa kike kupata mimba .Ametaja Wilaya ya Nkasi kuwa inaongoza kwa wasichana 25 kuripotiwa kushindwa kuendelea na masomo mwaka huu kutokana na mimba za utotoni.

WARATIBU WA PRESS CLUB ONGEZENI KASI KUFUATILIA VITENDO VYA UKIUKWAJI HAKI ZA BINADAMU

Image
Waratibu wa Klabu za Waandishi wa habari nchini (Press Clubs) wametakiwa kuongeza jitihada za kufuatilia matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya waandishi wa habari na kuripoti kwa ajili ya kuchukuliwa hatua. Akifungua mafunzo ya siku tatu kwa waratibu hao jana Jijini Dodoma, Afisa Programu kutoka klabu za waandishi wa habari nchini UTPC, Victor Maleko amesema waandishi wa habari wamekuwa wakikabiliwa na ukiukwaji wa haki za binadamu na kukwamisha utendaji wao wa kazi wa kila siku. Amesema UTPC kwa ushirikiano na shirika la IMS Denmark wameingia mkataba wa kusimamia ukiukwaji wa uhuru wa habari (madhila), ambayo ni moja ya haki za msingi za kidunia na waratibu kwa kuwa ni kiungo kikubwa wanatakiwa kuongeza juhudi za kuripoti matukio hayo ili kuyakomesha. Maleko amesema ili kufanikisha zoezi hilo UTPC imekuwa ikitoa mafunzo na midahalo mbalimbali ya ulinzi na usalama kwa mwandishi wa habari ikiwemo waratibu kujengewa uwezo wa kufwatilia madhila dhidi ya waandishi wa habari nch

TANROADS KUTOA MAFUNZO TABORA

Image
  Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mjini, Yahaya Nawanda, akimuelekeza jambo Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Tabora, Mhandisi Raphael Mlimaji, wakati akifungua semina ya mafunzo kuhusu Sheria ya Udhibiti Uzito wa Magari ya Afrika Mashariki ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018, mkoani Tabora.

DC NAWANDA AFUNGUA SEMINA YA MAFUNZO KWA WADAU WA USAFIRISHAJI

Image
  Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mjini, Yahaya Nawanda, akifungua Semina ya mafunzo kwa wadau wa usafirishaji (hawapo pichani), kuhusu Sheria ya Udhibiti Uzito wa Magari ya Afrika Mashariki ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018, mkoani Tabora.

BILIONI 18 KUANZA UJENZI WA BARABARA 3 GEITA

Image
  BILIONI 18 KUANZA UJENZI WA BARABARA 3 GEITA.   Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mheshimiwa Rosemary Senyamule, amesema kuwa Serikali imetenga jumla ya Shilingi Bilioni 18 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara tatu mkoani humo.   Ameyasema hayo wakati akifungua semina ya mafunzo kwa wadau wa usafirishaji kuhusu Sheria ya Udhibiti Uzito wa Magari ya Afrika Mashariki ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018 inayofanyika kwa siku moja mkoani humo.   “Katika Bajeti ya Serikali ya mwaka 2021/2022, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Ujenzi), kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), imetenga Shilingi Bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Nyamirembe hadi Katoke (Km 50), Bilioni 6 kwa ajili ya barabara ya Geita hadi Kahama (Km133), na Shilingi Bilioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa Barabara ya Geita hadi Nzega (Km 54),” amesema Senyamule.   Ameongeza kuwa barabara hizo tatu ambazo hadi sasa zimetengewa jumla ya shilingi Bilioni 18, zinaendelea na taratibu za ujenzi, vilevile kwa

SHERIA YA UTHIBITI UZITO WA MAGARI

Image
  M simamizi wa Mizani kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Leonard Saukwa, akitoa elimu kwa wadau wa sekta ya usafirishaji, kuhusu  ya Sheria ya Afrika Mashariki ya Udhibiti wa Uzito wa Magari ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018, mkoani Geita.

TANROADS GEITA WAZUNGUMZA NA WASAFIRISHAJI

Image
  Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Geita, Mhandisi Gladson Yohana akisoma taarifa yake kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita (hayupo pichani), kuhusu Semina ya Mafunzo ya Sheria ya Udhibiti Uzito wa Magari ya Afrika Mashariki ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018, mkoani Geita.

RC WA GEITA NA WADAU WA USAFIRISHAJI

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule, akifungua Semina ya mafunzo kwa wadau wa usafirishaji (hawapo pichani), kuhusu Sheria ya Udhibiti Uzito wa Magari ya Afrika Mashariki ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018, mkoani Geita.