Halmashauri Ya Kalambo Yafanikiwa Kupunguza Utapiamlo Kwa Watoto Chini Ya Miaka 5
Halmashauri ya Kalambo mkoani Rukwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 imefanikiwa kutekeleza mpango kabambe wa lishe wa taifa kwa kupunguza utapiamlo mkali kwa watoto chini ya miaka mitano.
Utekelezaji
wa mpango huo umekuwa ukitekelezwa na idara ya afya kwa kushirikina na idara
mtambuka ambazo ni kilimo, elimu msingi na elimu sekondari kwa kutoa elimu ya
lishe bora katika jamii kupitia vituo vya kutolea huduma za afya ikiwemo ulaji
wa vyakula vyenye virutubishi.
Mapema
akiongea kupitia kikao cha kamati ya lishe ya wilaya kilicho fanyika katika
ukumbi wa mkuu wa wilaya hiyo Robert Tepeli, alisema katika kipindi cha mwaka
wa fedha 2022/2023 Halmashauri ilifanikiwa kukagua vyakula na madini joto
ikiwemo chumvi zinazo uzwa madukani sambamba na unyweshaji Vitamin (A) na kutoa
dawa za minyoo kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya.
Alisema
katia kipindi hicho walifanikiwa kutekeleza zoezi la utoaji elimu kwa watoa
huduma za Afya juu ya utambuzi wa utapiamlo na matibabu kulingana na hali ya
utapiamlo.
‘’idara ya kilimo na mifugo inahusika moja kwa moja katika kutekeleza Afua za lishe kupitia kilimo na ufugaji ambapo katika kipindi hicho idara hiyo imefanikiwa kusimamia na kutoa elimu juu ya ufugaji bora wa samaki kwa wafugaji katika kata za Matai na Sundu na upandaji wa michikichi katika kata za Kasanga Mpombwe ili kuwezesha wananchi kunufaika na vitamin (A).’’alisema Tepeli.
Kwa
upande wake kaimu afisa elimu msingi wilayani humo Nhand Jilala alisema idara
hiyo imefanikiwa kutoa elimu na hamasa katika shule za msingi juu ya umuhimu wa
wanafunzi kupata chakula shuleni angalau mlo moja kwa siku ikiwa ni pamoja na kufuatilia
idadi ya shule ambazo zimekuwa zikitoa chakula kwa wanafunzi na kubaini shule
44 kati 99 kutoa huduma hiyo.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya hiyo Lazaro Komba alimwagiza afisa lishe wilayani
humo kuhakikisha afua zote za zilishe zinatekelezwa ikiwa ni pamoja na kutenga
fedha za utekelezaji.
Comments
Post a Comment