Dc Kalambo Ataka Walio Husika Kumuozesha Mwanafunzi Wa Darasa La Saba Kukamatwa

Mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Lazaro Komba ameliagiza Jeshi la polisi wilayani humo kuwakamata wazazi na walezi waliomwozesha mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Mbuza kata ya Mkowe mwenye umri wa miaka 17 na kumuozesha kwa Asulwa Sikombe mkazi wa kijiji cha Mbuza.

Taarifa kutoka kwa kwenye uongozi wa kijiji hicho akiwemo mwenyekiti wa kijiji hicho Alisen Machenchelwa na mkuu wa shule hiyo Fedelisi Mbuluko zimeeleza kuwa mwanafunzi huyo Mach 2023 alitoroka kwenye makazi ya wazazi wake na kutokomea kusiko fahamika na kwamba baada ya kurejea June 2023 wazazi wake walimua kumuozesha kwa ndugu Asulwa Sikombe mkazi wa kijiji cha Mbuza.

Walieleza kuwa baada ya kupata taarifa hizo waliamua kuwakamata wazazi wa binti huyo na kuwafikisha kwenye kituo cha polisi Matai kwa hatua zaidi.

Hata hivyo mapema akiongea ofisini kwake mkuu wa wilaya hiyo Lazaro Komba amesema mpaka sasa Jeshi la polisi linamsaka aliyeozeshwa mwanafunzi huyo na kwamba wazazi wawili wa mwanafunzi huyo wamekamatwa.

Licha ya hilo alitoa wito kwa wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwaozesha wanafunzi kwani ni kosa kisheria.

Comments

Popular posts from this blog

Wakulima Rukwa kutumia zana bora kuongeza uzalishaji wa mazao msimu mpya wa kilimo

UTPC KUENDELEA KUELIMISHA UMMA,UMUHIMU WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

MAENDELEO YA CHUO CHA UALIMU SUMBAWANGA