Watumishi Wa Umma Wilayani Kalambo Waungana Kuadhimisha Kumbukizi Ya Mashujaa Kwa Kufanya Usafi.
Watumishi wa Umma wilayani Kalambo mkoani Rukwa wameungana na watu wengine katika kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya mashujaa kwa kufanya usafi kwenye majengo ya hospitali ya wilaya hiyo ili kuendeleza kampeni ya usafi wilayani humo.
Zoezi hilo liliongozwa na Mkuu wa
wilaya hiyo Lazaro Komba alisisitiza kuwa zoezi hilo ni endelevu kwa kila siku
ya mwisho wa mwezi ili kukabiliana na magonjwa ya milipuko ikiwemo kipindupindu
na magonjwa ya kuhara.
Komba alisisitiza wananchi kujenga
mazoea kufanya usafi wa mazingira kuzunguma maeneo yao husika kwa lengo la
kuifanya wilaya kuwa safi muda na wakati wote.
‘’Kimsingi leo tumekutana kufanya usafi hapa kwenye majengo ya Hospitali ya wilaya Kalambo kama sehemu ya kuadhimisha kumbukizi ya siku ya mashujaa na maadhimisho haya kwa ngazi ya kitaifa yanafainyika mkoani Dodoma’’ alisema komba.
Mapema akiongea na Watumishi wa
umma wakati wa shughuli za usafi kwenye maeneo hayo ,Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri
hiyo Shafi Mpenda alisema Halmashauri
imeanzisha sheria ndogo ili kudhibiti uchafuzi wa mazingira ikiwemo kuhakikisha
kila mwananchi anakuwa na choo bora.
Comments
Post a Comment