KATIBU TAWALA AFANYA ZIARA WILAYA YA KALAMBO
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Bw.Gerald Kusaya amefanya ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya Kalambo.
Lengo la Ziara hiyo ni kukagua miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa Wilayani humo.Mradi aliyotembelea ni ujenzi wa Soko la kisasa la samaki utakaogharimu Tshs.Bilion 1.5 mpaka kukamilika kwake.
Ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kwa usimamizi mzuri wa ujenzi huo unaofanyika katika kata ya Kasanga.
Akizungumza katika eneo la mradi Katibu Tawala wa Mkoa ameeleza kuwa ujenzi wa Soko Hilo utasaidia wavuvi wanaoendesha shughuli zao katika ziwa Tanganyika kupata uhakika wa Soko la samaki,Hali itakayosaidia kuinua uchumi wa wavuvi hao na kuchangia ongezeko la makusanyo ya Mapato kwa Halmashauri ya Wilaya Kalambo.
Miradi mingine iliyokaguliwa ni pamoja na ujenzi wa shule mpya ya msingi Matai 'B' kupitia mradi wa BOOST,ujenzi wa madarasa mawili ya awali shule ya msingi kilewani kupitia mradi wa BOOST na ujenzi wa madarasa mawili shule ya msingi Kilewani kupitia fedha za ruzuku.
Katibu Tawala amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Bw.Shafi Mpenda kuhakikisha ujenzi wa madarasa hayo unakamilika kwa wakati na kwa ubora ili kutimiza malengo ya Serikali ya awamu ya sita kuboresha Mazingira ya kufundishia na kujifunzia.
Comments
Post a Comment