Posts

Showing posts from July, 2022

MRATIBU MSAIDIZI WA SENSA MKOANI RUKWA JAMES KAPENULO AKIELEZEA MATUMIZI YA VISHIKWAMBI KWA WAANDISHI WA HABARI

Image
  NA: FRANCO NKYANDWALE. SUMBAWANGA. Mratibu Msaidizi wa Sensa ya Watu na Makazi Mkoani Rukwa James Kapenulo akielezea matumizi ya vishikwambi kwa Wandishi wa Habari Mkoani Rukwa, amesema kuwa vishikwambi hivvyo vitatumika na makarani wa Sensa hiyo hapo tarehe 23.08.2022 na Makarani hao watapatiwa mafunzo jinsi ya kuvitumia na amefafanua kwamba, zoezi hilo ambalo litafanyika kidigitali na ni Sensa ya tofauti ikilinganishwa na Sensa zote zilizofanyika hapo awali. Ambapo taarifa za Kidemografia zitajazwa kwenye mfumo kupitia kishikwambi hali itakayoondoa upotevu wa taarifa muhimu za watu.

JARIBIO LA ZOEZI LA SENSA KUFANYIKA RUKWA

Image
  Na: FRANCO NKYANDWALE:. SUMBAWANGA.   Wananchi Mkoani Rukwa wametakiwa kujiandaa na zoezi la sensa litakalofanyika Mwezi Agost 23 mwaka huu kwa kuwepo kwenye kaya zao ili watoe ushirikiano kwa makarani wa sensa ili wahesabiwe kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla. Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa kijiji cha Luwa Kata ya Ntendo katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Saveri James alipokuwa akiongea na Rukwa press wakati makarani wa sensa walipotembelea kijijini hapo kwa lengo la kukagua miundo mbinu mbalimbali na mipaka ya kijiji. James amesema kuwa sensa ya watu na makazi ni muhimu kwa taifa lolote ambalo linaweka mipango na mahitaji muhimu kwa jamii yake na lengo la sensa hiyo ni kujua idadi ya watu na makazi na kuweka mipango ya namna serikali itakavyoendesha shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kuboresha miundo mbinu kwa manufaa ya wananchi.  Kwa upande wa baadhi ya wananchi wamesema wao wamejiandaa kuhesabiwa ambapo Mwanakijiji  Leonard Mikael ameshuhudia kuwa wapo tayari

VIJANA WA KIKRISTO WATAKIWA KUWA KIELELEZO KWA JAMII

Image
  NA: FRANCO NKYANDWALE SUMBAWANGA. Mwalimu Kitaaluma Joseph Shilingi wa Kanisa la Evangelist of God (T) Mashujaa wa Yesu Pito lililopo katika Halimashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ameyasema hayo wakati wa semina ya Vijana inayoendelea Kanisani hapo kuanzia Jumapili ambayo itakachukua muda siku tatu zaidi.  Amewataja Vijana kuwa ni nguzo muhimu ya Kanisa na kwa jamii kwa ujumla, amesema kuwa wapo baadhi ya Vijana wamejificha Kanisani na kufanya vitendo ambavyo havimpendezi Mungu. Mwalimu Shilingi amewashauri wazee wa Kanisa kufuatilia mwenendo wa Vijana ambao hawana msimamo wa imani ya kikristo wakalishwe chini na kuonywa mapema bila kufanya hivyo hapatakuwa na ndoa imara hapo baadaye na Kanisa litapoteza mwelekeo. Msingi wa Kanisa lolote ni kuwa na wakristo waliosimama kiroho, kimwili, kiuchumi, na kumtumikia Mungu wakiwa wasafi wa miili na mazingira yao kimaisha. Mwalimu Shilingi alisisitiza na kufafanua kwamba Vijana wajishulishe na biashara ndogo ndogo ili wasiwe tegemezi katika f

JIPANGENI ZAIDI KUHAKIKISHA WATU WANAJITOKEZA SIKU YA SENSA-ANNE MAKINDA-KAMISAA WA SENSA TANZANIA

Image
  Kamisaa wa sensa na Spika Mstaafu Anne Makinda amewataka viongozi wa mkoa wa Rukwa kujipanga kuhakikisha watu wengi zaidi wanajitokeza siku ya kuhesabiwa ifikapo Agosti 23 mwaka huu nchi itakapofanya zoezi la sensa ya watu na makazi.   Kiongozi huyo ametoa wito huo mjini Sumbawanga  wakati akizungumza na wadau kuhusu hali ya maandalizi ya sensa nchini pamoja na kutoa elimu ya umuhimu wa zoezi la sensa mwaka huu 2022.   Makinda alibainisha kuwa katika zoezi zoezi hili limejengwa katika msingi wa kiutawala ambapo utaratibu umewekwa  watu watahesabiwa pale alipolala.   " Tutahesabu watu wote mahala walipolala kama ni vituo vya mabasi, nyumba za wageni, katika kaya, waliopo hospitalini pia wale watakaokuwa kwenye magereza na mahabusu wote maharani wa sensa watawafikia kwa utaratibu uliowekwa na serikali" alisisitiza Mama Makinda.   Katika hatua nyingine Kamisaa huyo wa sensa alisema viongozi na jamii ya mkoa wa Rukwa ikumbuke umuhimu wa kutoa taarifa za walemavu

SENSA KWA MAENDELEO, JIANDAE KUHESABIWA

Image
 

Kukumbatia ujuzi wa Dijitali mustakabali wa uandishi wa habari.

Image
    Kukumbatia   ujuzi wa Dijitali mustakabali wa uandishi wa habari. Ulimwengu umeingia katika mfumo wa teknolojia iliyokuwa ,hivyo kupelekea kuachana na mfumo wa analojia na kwenda na dijital hii ina rahisisha namana nzuri ya mawasiliano,pamoja na upatikanaji wa taarifa   mbalimabali ndani na nje ya nchi,pia ni mabadiliko ambayo yanaendana   sambamba na ubunifu wa kidijital Ujuzi wa kidigitali ni uwezo wa kutumia mbinu mpya za kiteknolojia katika kutatua matatizo ya kiutendaji katika   nafasi za uandishi wa habari na kupata matokeo chanya yanayomfanya kutambulika katika ulimwengu wa digitali. Asha Abinallah ni kiongozi wa kampuni   ya media convergency inayotoa mafunzo kwa waandishi wa habari wanawake kuhusu uandishi wa kidigitali ikiwa na lengo la kuwaendeleza waandishi   wa habari katika uandishi wa habari kutumia teknolojia iliyokuwa. Amesema   kupitia program hiyo maalumu ya mafunzo ya ujuzi kidigitali inawapa waandishi kupata uelewa na ujuzi wa namna ya kuandaa na kute

DC TANO MWERA AAGIZA WAKANDARASI RUWASA KUJENGA MIRADI KWA KIWANGO KINACHOTAKIWA

Image
  DC TANO MWERA AAGIZA WAKANDARASI RUWASA KUJENGA MIRADI KWA KIWANGO KINACHOTAKIWA KALAMBO-RUKWA Mkuu wa wilaya ya Kalambo iliyopo Mkoani Rukwa TANO MWERA amewataka wakandarasi na wasimamizi wa RUWASA wilayani humo kuhakikisha Miradi ya maji pamoja na miundombinu yake inajengwaa kwa kiwango kitakachowezesha miradi ya maji kudumu kwa mda mrefu ili kupunguza changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi. Ameleeza hayo baada ya kuambatana na kamati ya usalama wilayani humo kwa lengo la kukagua Miaradi ya maji  inayojengwa katika vijiji vya Luse,Kalaela na Kalemasha inayofadhiliwa na fedha za uviko na P4R , huku  FRANCIS MAPUNDA kutoka kitengo cha Uhandisi RUWASA Kalambo akieleza maendeleo ya miradi hiyo. Aidha Kamanda wa TAKUKURU Wilayani humo LUPAKISYO MWAKYOLILE ametoa wito kwa RUWASA kuweka utaraibu mzuri wa Kulinda miundombinu ya maji ili iweze kudumu kwa mda mrefu na kusimamia ipasavyo makusavyo ya bili za maji huku wananachi wakipongeza hatua ya kufikiwa na

MAENDELEO YA CHUO CHA UALIMU SUMBAWANGA

Image
  CHUO CHA UALIMU SUMBAWANGA CHAFIKIA 64% KUJENGWA Na. OMM Rukwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imepongezwa kwa kuwezesha upatikanaji  fedha shilingi 3,852,697,911 zinazotumika katika awamu ya kwanza kujenga majengo 11 ya chuo kipya cha Ualimu Sumbawanga eneo la Pito ambapo mradi huo umefikia asilimia 64 hadi sasa. Akizungumza leo (06. 07.2022) kwenye ukaguzi wa mradi huo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti aliwaeleza waandishi wa habari kuwa serikali inatekeleza mradi huo kwa lengo la kufungua fursa za kielimu kwa wananchi ambapo utakapokamilika utasidia kuchochea ukuaji wa uchumi. "Rukwa tumenufaika na mradi huu wenye thamani ya shilingi Bilioni 3.9 ambapo majengo kadhaa yamekamikika na mengine jitihada za ukamilishaji zinaendelea vizuri. Nimeridhishwa na  kazi inayoendelea hapa na kuhusu changamoto chace nitawasiliana na Wizara ya Elimu tuzitatue mapema na mradi ufike mwisho" ,alisema Mkirikiti.  Katika hatua nyingine Mkuuu huyo wa Mkoa alip

VIJANA WANATAKIWA KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUJIPATIA KIPATO.

Image
  NA: Franco NKYANDWALE SUMBAWANGA.              VIJANA WANATAKIWA KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUJIPATIA KIPATO . Vijana watakiwa kutumia mitandao ya kijamii kujiinua kiuchumi zama hizi za teknolojia na utandawazi badala ya kukaa vijiweni huku wakiilalamikia serikali kuwa hakuna ajira. Hayo yameelezwa leo na Mhubiri Enala Malila wakati wa siku ya kuadhimisha sikukuu ya vijana kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Usharika wa Luther Dayosisi ya Ziwa Tanganyika katika Manispaa ya Sumbawanga. “Wapo baadhi ya vijana ambao humiliki simu janja kubwa na zenye gharama ambazo huzitumia kuchati na kuangalia mambo ambayo huwapotosha kimamaadili, badala ya kuzifanya simu hizo kuwa mtaji ambapo wangewaza kutangaza biaashara zao ndogondogo wanazozifanya mitaani kwao,” Malila alifafanua. Mzee wa Kanisa Mariamu Ndongokazialisoma somo la pili kutoka kwenye kitabu cha 1Timotheo 4:11-16, Mhubiri Malila alifafanua zaidi kuwa ili kijana aweze kufanikiwa kichumi ni lazima kijana aweze