Posts

Showing posts from January, 2023

PLAN INTERNATIONAL YACHANGIA VIFAA VYA ELIMU RUKWA

Image
    Shirika la Plan International Tanzania limekabidhi msaada wa vitabu, vyoo shirikishi na miundombinu ya maji kwa shule za sekondari na msingi kwenye Halmashauri za Wilaya   Nkasi, Kalambo na Sumbawanga vyenye thamani ya shilingi Milioni 786 .   Halfa ya makabidhiano ya msaada huo imefanyika katika shule ya msingi Milundikwa wilaya ya Nkasi jana (Januari 19,2023) ambapo Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Sebastian Waryuba alipokea msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga.   Waryuba akizungumza kwenye hafla hiyo alitoa pongezi kwa shirika hilo kwa kuchangia vyoo shirikishi 17 na miundombinu ya maji katika shule za msingi 7 na sekondari 9 katika Wilaya za Nkasi, Sumbawanga Vijijini na Kalambo vyenye jumla ya thamani ya shilingi   za kitanzania 716, 607, 527.     Plan International imetoa pia   vitabu vya kiada 10, 128 kwa shule za msingi 29   za wilaya ya Nkasi vyenye thamani ya shilingi za kitanzania 70, 210, 000 vitakavyotumika kufundishia na kujifunzia wa

WATATU MBALONI UTAPELI KIMTANDAO

Image
  WATATU MBALONI UTAPELI KIMTANDAO Jeshi la Polisi Mkoani Rukwa limewakamata wauhumiwa watatu(3)wanaume wakazi wa Sumbawanga amabo   wanaojihusisha na uhalifu wa kimtandao kwa njia ya kupiga simu na kuwatishia watu kwa nia ya kujipatia kipato. Akitoa taarifa   Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa ACP- Shadrack Masija amesema wimbi la utapeli kupitia mtandao Mkoani Rukwa limekuwa likiongezeka na kusema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kujiimarisha na kuhakikisha wanatokomoeza utapeli wa kimtandao wa aina yotote ili kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani na utulivu. Aidha Katika hatua nyingine Kamanda Masija amesema kumekuwepo na matukio mbalimbali ya watu kupoteza maisha kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha Katika Mkoa wa Rukwa mabapo Katika Wilaya ya Nkasi kumetokea vifo vya watu wawili akiwemo mwanafunzi mmoja na mvuvi mmoja,Wilaya ya kipolisi Laela kumetokea kifo cha mtu mmoja aliyetumbukia kwenye dimbwi lililojaa maji baada ya mvua kubwa kunyesha na kupelekea kifo chak

SERIKALI KUWEKA NGUVU ZAIDI UTUNZAJI WA MAZINGIRA

Image
  SERIKALI KUWEKA NGUVU ZAIDI UTUNZAJI WA MAZINGIRA Na Peter Helatano-Rukwa Katika miaka kadhaa suala la utunzaji wa mazingira kwa jamii ya Mkoa wa Rukwa lilisahaulika sana,Ukataji miti kiholela,Uchomaji Mkaa kwa kasi,Ufanyaji wa shughuli za kilimo zinazohusisha ukataji miti kwa wingi bila kurejesha miti iliyokatwa, Kulima na kufanya shughuli nyingine kwenye milima na Kuchungia mifugo mingi bila uthibiti wa idadi ya mifugo kwenye maeneno muhimu hasa vyanzo vya maji lilikuwa ni suala la kawaida na baadhi ya wananchi hawakujali athari za hayo yote kwa wakati ujao.  IMEELEZWA kuwa kupitia biashara ya hewa ya ukaa wakazi wake vijiji nane katika  katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi wamepokea zaidi ya Sh bilioni 6.5/- kati ya Julai na Disemba 2022. Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Makamu was Rais - Mazingira,Dk Switbert Mkama alibainisha yao jana alipokuwa akifungua warsha ya siku mbili iliyofanyika mjini Sumbawanga iliyoratibiwa na Mradi Endelevu wa Mazingira na Uhifa

WANANCHI WATAKIWA KUPANDA MITI KUTUNZA MAZINGIRA.

Image
  WANANCHI WATAKIWA KUPANDA MITI KUTUNZA MAZINGIRA. Wananchi mkoani Rukwa wametakiwa kuacha tabia ya kukata miti ovyo na kufanya shughuli za kilimo kwenye vyanzo vya maji Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Rukwa Queen Sendiga   alipotembelea ofisi ya klabu ya waandishi wa habari mkoani Rukwa na kuwataka   kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi yao Sendiga amesema anatarajia kupokea miche ya miti milioni moja ambayo tayari imeandaliwa na   Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Mkoa wa Rukwa na itapandwa kwenye kingo za barabara na kwenye vyanzo vya maji. Aidha amewataka watendaji wa kata na vijiji kwenye maeneo yao kuhakikisha wanasimamia zoezi la upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira. Katika hatua nyingine Sendiga amesema atahakikisha waandishi wa habari wanashirikiana na taasisi nyingine Katika kuutangaza Mkoa wa Rukwa na kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira.

SERIKALI KUONGEZA WIGO MAWASILIANO MIPAKANI

  SERIKALI KUPANUA WIGO WA MAWASILIANO MIPAKANI Serikali kupanua wigo wa Mawasiliano Katika Mikoa iliyopo mpakani mwa nchi nyingine jirani ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya Mawasiliano kwa wananchi na kuondoa vikwazo vya kimtandao kwa kushirikiana na makampuni mengine ya Mawasiliano kupitia mfuko wa huduma ya Mawasiliano kwa wote kwa kujenga minala ya Mawasiliano sehemu zenye changamoto ya mtandao. Ziara ya Waziri wa Habari,Mawasiliano  na teknolojia ya habari Mkoani Rukwa wilayani Kalambo  Nape Mnauye imebeba undani wa suala la Mawasiliano Katika uzinduzi wa mnala wa Mawasiliano uliofanyika Katika kijiji cha Katuka. Hatua hiyo ya kuwekwa mnala Katika kijiji cha Katuka imepongezwa na wananchi huku Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga akibainisha maeneo yenye changamoto za kimtandao

Waziri Bashe akiri Matumizi ya mbolea Mkoa wa Rukwa yameongezeka

Image
  *Waziri Bashe akiri Matumizi ya mbolea Mkoa wa Rukwa yameongezeka*  Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ameeleza kuwa, matumizi ya mbolea kwa mkoa wa Rukwa msimu huu wa kilimo(2022/2023) yameongezeka tofauti na msimu wa kilimo 2021/2022. Alisema,  matumizi ya mbolea kwa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kwa msimu wa kilimo 2021 ilikuwa ni tani 1600 lakini msimu wa kilimo 2022/2023 kuanzia  tarehe 15 Agosti, 2022  mpaka tarehe 3 Januari 2023 kiasi cha tani 842 sawa na asilimia 50 ya mbolea zilizotumika msimu uliopita wa kilimo kimetumika.  Amebainisha matumizi  ya mbolea kwa msimu uliipita yanalingana na matumizi ya mbolea kwa nusu msimu wa mwaka 2022/23 japo msimu wa kilimo bado unaendelea na kubainisha muitikio wa matumizi ya mbolea umekuwa mkubwa kutokana na bei za mbolea kushuka pamoja na kupanda kwa bei ya nafaka kulikowafanya wakulima kuongeza mashamba  yao ya kulima. Waziri Bashe amebainisha hayo jana tarehe 4 Januari, 2023 alipokuwa katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya siku m