KASULU DC YAENDELEZA UUNDAJI WA KLABU ZA LISHE

 Na Mwandishi wetu.

Katika kuendelea kuboresha Afya ya Jamii Halmashauri ya Wilaya Kasulu kupitia kwa wataalamu wa lishe inaendelea kuunda Klabu za lishe mashuleni ambazo zitasaidia kutoa Elimu ya masuala ya lishe,kwa kuanzisha bustani za mbogamboga na matunda.


Akitoa ripoti hiyo Leo katika kikao Cha lishe kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo Afisa Lishe Kingolo Sayi amesema Hali ya uwepo wa Klabu za lishe ni asilimia 43 kwa shule za msingi na asilimia 75 kwa shule za sekondari.


Sayi ameongeza kuwa katika kuimarisha uungwaji wa Klabu hizo mashuleni,vijiji 24 katika kata 15 vimehamasishwa juu ya umuhimu wa Klabu shuleni.


Itakumbukwa kuwa uwepo wa Klabu za lishe shuleni zinasaidia kutoa Elimu kwa wanafunzi a jamii juu ya umuhimu wa lishe Bora na ushiriki wake.


Comments

Popular posts from this blog

Wakulima Rukwa kutumia zana bora kuongeza uzalishaji wa mazao msimu mpya wa kilimo

UTPC KUENDELEA KUELIMISHA UMMA,UMUHIMU WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

MAENDELEO YA CHUO CHA UALIMU SUMBAWANGA