SERIKALI,VIONGOZI WA DINI WATETA LUGHA MALEZI YA WATOTO

 Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, wanawake na Makundi maalumu,John Jingu amesema kuwa migogoro ya kifamilia inachangia watoto kuwa katika Hali mbaya ya MALEZI na kuongeza vitendo vya ukatili kwa watoto.



Dkt.Jingu amesema,Takwimu za jeshi la polisi Tanzania kuanzia Januari mpaka disemba 2022,kulikuwa na matukio 12,163 ya ukatili ambapo ubakaji ni 6,335,ulawiti ni 1,557 na mimba za utotoni ni 1,555 kwa mujibu wa jeshi la polisi.


Akizungumza jijini Dar es salaam Julai 17,2023 katika mkutano wa viongozi wa dini na Serikali,Jingu amesema hadi kufikia machi,2023 watoto wanaoitwa wa mitaani walikuwa 335,971,kati Yao wakiume 168,634 na wakike 167,337 na walibainishwa kuishi katika Mazingira hatarishi.

"Jumla ya watoto 2,185 kati Yao wa kiume 1,324 na wakike 861 walikuwa wanafanya kazi na kuishi Mitaa ,baadhi Yao waliunganishwa na familia zao Serikali imeratibu uanzishwaji wa makao ya watoto 333 ya Serikali na binafsi ambayo yanahifadhi watoto 12,077


Ameongeza kuwa kwa Sasa wanashuhudia migogoro mingi ya ndoa katika familia ambapo watoto Huwa ndio waathirika wakubwa huku Takwimu za Wizara za Julai 2022 had April 2023 zikionesha jumla ya mashauri 1,574 ya migogoro ya ndoa na familia ilipokelewa kwenye mabaraza ya usuluhishi ya ndoa kutoka ngazi za Halmashauri na wizarani.

"Kati ya mashauri hayo 895 yalifanyiwa usuluhishi na mashauri 679 yalipatiwa Rufaa ya kwenda mahakamani"alisema Dkt.Jingu.

Jingu amesema kufuatia Hali hiyo Serikali imeandaa muongozo unaoelekeza namna Bora ya malezi ya watoto na familia kwa kuzingatia Mazingira yetu kwa kusisitiza zaidi wajibu wa wazazi au walezi katika malezi ya watoto na familia.
 
Mwongozo huo wa kitaifa unajulikana la familia Bora,Taifa imara.Mwongozo wa Taifa wa mujibu wa wazazi na walezi katika malezi ya watoto na familia wa mwaka 2023.Lengo la mwongozo huo ni kujengeana uelewa na uzingatiaji wa masuala ya msingi kama Taifa juu ya wajibu wa wazazi au walezi kwenye malezi ya watoto na Familia.

Alisema mwongozo huo una nguzo kuu tatu ambazo ni Kali,Linda na wasiliana au zungumza ambapo zaidi ni kujenga muunganiko na mtoto.





Comments

Popular posts from this blog

Watumishi Wa Umma Wilayani Kalambo Waungana Kuadhimisha Kumbukizi Ya Mashujaa Kwa Kufanya Usafi.

Dc Kalambo Ataka Walio Husika Kumuozesha Mwanafunzi Wa Darasa La Saba Kukamatwa

Mkurugenzi UTPC awataka Waandishi kuandika Habari za Usawa wa kijinsia ili kuleta mabadiliko Chanya katika jamii.