HUDUMA YA KITI MWENDO YAANZISHWA KITUO CHA DALADALA MUHIMBILI.

 Hospital ya Muhimbili imeanzisha huduma ya kubeba wagonjwa wasioweza kutembea kutoka kwenye kituo Cha daladala kilichopo nje ya geti la kuingilia hadi katika maeneo ya kutolea huduma kwa kutumia Viti mwendo(wheel chairs).

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za uuguzi na ukunga wa MNH,Bi.Redempta  Matindi amesema kuwa huduma hiyo ni muhimu kwa kuwa wapo wagonjwa wasiojiweza kabisa kutembea wenyewe.


"Sisi kama watoa huduma tumeona ni vema kuanzisha huduma hii kuwasaidia mwendo wagonjwa ili wafike kwenye maeneo ya kutolea huduma wakishafika huko wanakutana na watoa huduma wa maeneo husika"amesema Bi Redempta.

Amesema huduma hizo zinatolewa na waliokuwa waraibu wa dawa za kulevya ambao wanaendelea na tiba ya Methadone ili kuwasaidia kurejea katika maisha ya kawaida.

Comments

Popular posts from this blog

Watumishi Wa Umma Wilayani Kalambo Waungana Kuadhimisha Kumbukizi Ya Mashujaa Kwa Kufanya Usafi.

Dc Kalambo Ataka Walio Husika Kumuozesha Mwanafunzi Wa Darasa La Saba Kukamatwa

Mkurugenzi UTPC awataka Waandishi kuandika Habari za Usawa wa kijinsia ili kuleta mabadiliko Chanya katika jamii.