Posts

Showing posts from August, 2023

Mtumishi Halmashauri Ya Kalambo Mbaroni Kwa Kukutwa Na Mashine Bandia Ya Ukusanyaji Mapato.

Image
   Na Baraka Lusajo - Kalambo  Jeshi la polisi Mkoani Rukwa linamshikilia Timoth Ngambeki ambae ni mtumishi wa Halmashauri ya Kalambo kwa tuhuma za kutumia mashine bandia na kutoa risiti feki kwa wananchi na kuisababishia serikali hasara ya shilling million thelathini na tisa na laki tano. Mapema akiongea ofisini kwake mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Kalambo Shafi Mpenda alisema mtumishi huyo aligundulika kufanya kitendo hicho baada ya kushindwa kuwasilisha fedha Benk na kwamba baada ya ufuatiliaji zaidi kwenye mageti ya ukusanyaji mapato aligundua uwepo wa udanganyifu kwenye utoaji wa risiti. ‘’baada ya kugundua uwepo wa udanganyifu kwenye swala la ukusanyaji mapato nilianzisha utaratibu wa kuweka madaftari ya kusaini kwenye mageti yote yanayo unganisha halmanshauri za jirani na kuweka watu ambao walikuwa wakifanya kazi ya kupiga picha risiti za ushuru kisha kunitumia na wakati mwingine nilikuwa nikiamka usiku na kufuatilia mwenendo wa ukusanyaji mapato kwenye mageti.’’alisema

Mkurugenzi UTPC awataka Waandishi kuandika Habari za Usawa wa kijinsia ili kuleta mabadiliko Chanya katika jamii.

Image
  Na.Neema Mtuka Mkurugenzi Mtendaji wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania(UTPC) Bw.Kenneth Simbaya amewataka Waandishi wa Habari kuendelea kuandika Habari za Usawa wa kijinsia ili kuleta mabadiliko Chanya kwa jamii. Simbaya ameyasema hayo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari za Usawa wa kijinsia yaliyo wakutanisha Waandishi wa Tanzania Bara na visiwani. Ameongeza kuwa Waandishi wanapaswa kuibua Habari za ukatili wa kijinsia ambazo zitasaidia jamii kubadili mitazamo hasi na kuachana na Mila potofu zilizopitwa na wakati ambazo Bado Zina mkandamiza mwanamke na kupotea maana ya Usawa wa kijinsia  Aidha amesema Waandishi wa Habari washirikiane kwa pamoja katika kuibua mambo mbalimbali yahusuyo jamii na kufanya kazi kwa pamoja na kuhakikisha wanazingatia maadili ya uandishi wa Habari kanuni na taratibu zilizopo. Mafunzo ya Usawa wa kijinsia yanafanyika mjini Morogoro ambapo pamoja na mambo mengine Waandishi wanatazamia kuleta mabadiliko makubwa katika jam