MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA SUMBAWANGA AFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI YA AFYA NA ELIMU.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Sumbawanga Bi.Lightness Msemo akiambatana na wataalamu toka ofisini kwake wamefanya ziara ya kukagua miradi ya Elimu na Afya pamoja na kufanya vikao na watumishi wa kata sita  mfinga,Mwadui,Kikwale,Kalumbaleza,Muze,Mtowisa,Zimba na Milepa.


Katika ziara hiyo alitembelea shule ya msingi kizumbi iliyopo katika kata ya Muze na kukagua ujenzi wa miundombinu ya vyoo inayoendelea katika shule hiyo.Katika kikao kazi Cha walimu na viongozi wa Kijiji akiwepo Mtendaji na mwenyekiti alisisitiza suala la kuwahi kazini kwa watumishi na kusimamia miradi inayoendelea kujengwa kwa ufanisi ili kuwa na Tija kwa jamii.


Pia alifanya ukaguzi katika Kijiji Cha Kasekela kata ya Mfinga baada ya ukaguzi wa mradi Mganga Mkuu wa wilaya Dr.Msuya akitoa Elimu kwa wazazi juu ya lishe Bora na kuwasihi wazazi kuzingatia lishe borakwa watoto ili kupunguza suala la udumavu kwa watoto.Mganga Mkuu aliwasihi wauguzi kuendelea kufanya kazi kwa kujituma ili kuendelea kuokoa maisha ya wanakasekela.


Aidha,Mkurugenzi alitembelea ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Maenje na kukagua ujenzi wa vyoo ambapo kwa ujumla ameridhishwa na ujenzi I nayoendelea,na kuwasihi mafundi waongeze kasi ya ujenzi ili kumaliza kwa wakati na kukabidhi majengo hayo.





Comments

Popular posts from this blog

Wakulima Rukwa kutumia zana bora kuongeza uzalishaji wa mazao msimu mpya wa kilimo

UTPC KUENDELEA KUELIMISHA UMMA,UMUHIMU WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

MAENDELEO YA CHUO CHA UALIMU SUMBAWANGA