Watoto 80,486 Kufikiwa Na Kamapeni Ya Chanjo Ya Polio Wilayani Kalambo
Na Baraka Lusajo - Rukwa
Ofisi ya Rais TAMISEM kwa kushirikina na wizara ya afya imepanga kuendesha kamapeni ya polio kwa mikoa minne inayopakana na nchi za Zambia ikiwemo mkoa wa Rukwa,katavi , Songwe na Mbeya ili kuwakinga watoto chini ya miaka 5 dhidi ya ugonjwa huo.
Hayo
yamebainishwa na kaimu mganga mkuu wa Halmashauri ya Kalambo Dr.Emmanuel
Kisyombe kupitia kikao cha kamati ya afya ya msingi (PHC) kilicho fanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo June 6/2023,Ambapo
amesema kampeni hiyo inarajiwa kuanza Julai 27/2023 na kuhitimishwa Julai
30/2023.
‘’Chanjo
ambayo itatumika katika kampeni hii ni chanjo ya polio ya sindano (IPV) ambayo
ina mpa kinga mtoto dhidi ya polio virus type 2’’na kwamba zaidi ya watoto
80,486 wanatarajiwa kufikiwa kupitia kampeni hiyo’’ alisema Dr Kisyombe.
Mapema
akiongea kupitia kikao hicho mkuu wa wilaya hiyo Lazaro Komba aliwataka wataalamu
wa afya wilayani humo kuendelea kushirikina na wadau wakiwemo viongozi wa dini
katika kudhibiti ugonjwa kwa kutoa elimu kwenye maeneo ya mikusanyiko, makanisani
na misikitini ili kuwezesha watoto wengi zaidi kupata chanjo hiyo.
Hata
hivyo imeelezwa kuwa polio ni ugonjwa unao sababisha ulemavu na tishio la
maisha unatokana na maambuzi ya virus vya polio na kwamba dalili zake ni pamoja
na maumivu ya kichwa, mwili kuchoka, kuchefuchefu na maumivu ya tumbo.
Comments
Post a Comment