Msimamo wa Nchi ni kulinda Uhuru wa Vyombo vya Habari
Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhe.Nape Nnauye amesema msimamo wa thabiti wa Nchi ya Tanzania ni kulinda Uhuru wa Vyombo vya Habari,na ndio mana Serikali iliamua kufanya marekebisho ya Sheria ya huduma ya Habari Sura ya 229,ili ikidhi Uhuru wa vyombo vya Habari. Mhe .Nape amesema hayo Leo Julai 31,2023 jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua kozi fupi ya 15 ya Wahariri wa vyombo vya Habari inayotolewa na chuo Cha Taifa Cha Ulinzi. "Wanahabari niwahakikishieni msimamo thabiti wa Nchi yetu ni kulinda Uhuru wa vyombo vya Habari.Mh.Rais mara nyingi amekuwa akiagiza kufanya kazi bila kuingilia Uhuru wa vyombo vya Habari",amesema Mh.Nape. Aidha amewataka Wahariri hao mara watakapomaliza kozi hiyo na kurudi katika vituo vyao vya kazi,wafanye kazi kwa kuangalia maslahi ya nchi,vilevile amewataka kuendelea kulifanya Taifa kuwa kitu kimoja na Kukuza Umoja wa Taifa. Kwa upande wake kansela wa chuo Cha Taifa Cha Ulinzi,Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee amesema kuwa mafu