MUNGU AMEKUCHAGUA HATUNA BUDI KUMUOMBA



  Na Franco NKYANDWALE

Sumbawanga


1. Frola (1966-2021 ) umejitenga kimapenzi na Nswima, Mungu amekuchagua.


2. Hakufanya kwa hiyari,

bali kama ua ulichanua na sasa limefunga kabisa.


3. Jicho la Nswima lina chozi chepechepe wa kufuta hakuna, ila MAULANA mfariji.


4. Naandika nikitetema leo yako Frola, umetangulia mbele ya haki, baadaye yetu zamu tutaonana.


5. Ndoa mliifunga, sasa kifo kimetengua Nswima moyoni amepwaya na kuwaya waya.


6. Frola bado jamii inakuhitaji mola kasema basi, Mungu amjazi faraja Nswima na familia.


7. Kila kona ni kilio hata kule Karema watu walia upweke umetuachia wategemezi ni machozi,TANZANIA yalia.


8. Mengi ulitenda kwa wema na faraja, leo tumejawa na simanzi, yako umemaliza ukurasa umefunga Frola.


9. Hakuna wa kutangua kifo hicho, kwa sote hatukwepi mioyo yetu imekinunia kifo, lakini hakuna namna.


10. Kwa mola utangulie, nawe ujuwe kwetu ni majonzi kwa Nswima ni zaidi. BURIANI Frola. 


11. Majukumu na upweke Frola umemwachia Nswima, nafsini hatakusahau kamwe,

Jamii inaomboleza.

Comments

Popular posts from this blog

Watumishi Wa Umma Wilayani Kalambo Waungana Kuadhimisha Kumbukizi Ya Mashujaa Kwa Kufanya Usafi.

Dc Kalambo Ataka Walio Husika Kumuozesha Mwanafunzi Wa Darasa La Saba Kukamatwa

Mkurugenzi UTPC awataka Waandishi kuandika Habari za Usawa wa kijinsia ili kuleta mabadiliko Chanya katika jamii.