Visit Kalambo water falls



 Na Peter Helatano

Visit to Kalambo water falls...Tembelea Mapolomoko ya maji Kalambo

Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Tano Mwera amesema maandalizi kwa ajili ya ziara ya kutembelea kivutio cha utalii cha maporomoko ya maji ya Kalambo yamekamilika na kuwa sasa yatafanyika tarehe 18 Desemba mwaka huu lengo ikiwa kukuza utalii wa ndani ya Mkoa wa Rukwa .

Mwera ametoa taarifa hiyo leo mjini Sumbawanga alipoongea na wanahabari.Ikumbukwe Kalambo water Falls Ni Mapolomoko ya Pili kwa ukubwa kutoka Yale ya Afrika kusini.Pia ina vivutio vya misitu ya Asili,Hifadhi na Maeneo ambayo yanavutia kiutalii.Yapo maeneo ya kuweka makambi kwa ajili ya kuchoma Nyama,ngoma,Kuogelea, Jogging na Burudani mbalimbali huku ukilitazama jua la kuzama kwa uzuri(Sun set) kupitia ziwa Tanganyika,ziwa lililojaa Samaki wenye Radha ya kipekee barani Afrika.Maji yake meupe yenye kukuwezesha kuona kina kwa chini na kukupa urahisi Kuogelea.Tembelea maeneo hayo usiishie tu kusimuliwa.

Comments

Popular posts from this blog

Watumishi Wa Umma Wilayani Kalambo Waungana Kuadhimisha Kumbukizi Ya Mashujaa Kwa Kufanya Usafi.

Dc Kalambo Ataka Walio Husika Kumuozesha Mwanafunzi Wa Darasa La Saba Kukamatwa

Mkurugenzi UTPC awataka Waandishi kuandika Habari za Usawa wa kijinsia ili kuleta mabadiliko Chanya katika jamii.