MWONGOZO WA KUPAMBANA NA RUSHWA KWA VIJANA WA SKAUTI RUKWA
MWONGOZO WA KUPAMBANA NA RUSHWA KWA VIJANA WA SKAUTI RUKWA
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Joseph Mkirikiti leo amekabidhiwa mwongozo wa kupambana na rushwa kwa vijana wa skauti mkoa wa Rukwa kwenye hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Sumbawanga.
Akikabidhi Mwongozo huo ,Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Rukwa Bw. Daniel Ntera alisema lengo la serikali ni kuona vijana wakifundishwa njia mbalimbali za kukabiliana na rushwa wakiwa mashuleni.
Mwongozo huo utatumika kwa vijana wa skauti kuanzia shule za msingi, sekondari hadi vyuo ambapo pia walimu watatumika kufundishia elimu ya kudhibiti na kupambana na rushwa kwenye jamii ya watanzania.
Comments
Post a Comment