DKT.MOLLEL AHIMIZA KUWASAIDIA WANANCHI WENYE MAHITAJI


 Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel ameuagiza uongozi wa Afya Mkoa wa Tanga chini ya Mganga Mkuu wa Mkoa huo kuhakikisha Kijana Elias Mgomela (27) mkazi wa Jijini Tanga kupelekwa haraka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufanyiwa upasuaji wa uvimbe alionao shavuni.

Elias amekuwa akiishi na uvimbe huo toka mwaka 2007 baada ya kukosa fedha za matibabu na amekuwa akifanya shughuli za kuimba na kucheza katika vikundi vya ngoma vya uelimishaji na uburudishaji jamii ndani ya Jiji la Tanga.

Dkt. Mollel ameihimza jamii kuendelea kusaidia wananchi wenye mahitaji ya kupata tiba kama wanavyochangia kwenye shughuli nyinginezo kama vile harusi na misiba.

Comments

Popular posts from this blog

WALIOFUKUA KABURI WAKAMATWA NA JESHI LA POLISI RUKWA

TAKUKURU YAIMARISHA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA KATIKA KONGAMANO LA 5 LA GLOBE NETWORK NCHINI CHINA

RC SENDIGA: TUTAFANYA MAPINDUZI YA KILIMO RUKWA