RED CROSS WATAKIWA KUANDAA MAFUNZO YA UOKOAJI MASHULENI


 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa  Joseph  Mkirikiti leo amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Chama cha Red Cross Mkoa wa Rukwa  ambapo amewataka waandae programu ya maokozi kwenye shule za Rukwa ili vijana wengi wawe na umahili wa kuokoa jamii pale majanga yanapotokea.


Mkirikiti amesema hayo leo ofisini kwake mjini Sumbawanga pia ameupongeza uongozi wa Red Cross kwa kazi wanayoendelea kuifanya kwenye jamii ya Rukwa huku akiwataka wawe na ushirikiano na Skauti pamoja na Jeshi la Zimamoto.


"Hamasisheni kampeni ya Damu Salama kwenye mkoa wetu mkishirikiana na Hospitali zetu za Halmashauri hususan maeneo ya vijijini hatua itakayosaidia kuokoa maisha ya watu " alisema Mkirikiti 


Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti  wa Red Cross Rukwa Saada Kimanta ameomba ushirikiano na uongozi wa mkoa ili watambulike na kupewa kipaumbele kwenye utekelezaji wa malengo ya Red Cross.


Aliongeza kusema Red Cross tunahitaji kushirikishwa kwenye shughuli za mkoa na kitaifa ikiwemo ziara za viongozi wa kitaifa pia shughuli za usafi na uokoaji.

Comments

Popular posts from this blog

Wakulima Rukwa kutumia zana bora kuongeza uzalishaji wa mazao msimu mpya wa kilimo

UTPC KUENDELEA KUELIMISHA UMMA,UMUHIMU WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

MAENDELEO YA CHUO CHA UALIMU SUMBAWANGA