MUNGU AMEKUCHAGUA HATUNA BUDI KUMUOMBA
Na Franco NKYANDWALE Sumbawanga 1. Frola (1966-2021 ) umejitenga kimapenzi na Nswima, Mungu amekuchagua. 2. Hakufanya kwa hiyari, bali kama ua ulichanua na sasa limefunga kabisa. 3. Jicho la Nswima lina chozi chepechepe wa kufuta hakuna, ila MAULANA mfariji. 4. Naandika nikitetema leo yako Frola, umetangulia mbele ya haki, baadaye yetu zamu tutaonana. 5. Ndoa mliifunga, sasa kifo kimetengua Nswima moyoni amepwaya na kuwaya waya. 6. Frola bado jamii inakuhitaji mola kasema basi, Mungu amjazi faraja Nswima na familia. 7. Kila kona ni kilio hata kule Karema watu walia upweke umetuachia wategemezi ni machozi,TANZANIA yalia. 8. Mengi ulitenda kwa wema na faraja, leo tumejawa na simanzi, yako umemaliza ukurasa umefunga Frola. 9. Hakuna wa kutangua kifo hicho, kwa sote hatukwepi mioyo yetu imekinunia kifo, lakini hakuna namna. 10. Kwa mola utangulie, nawe ujuwe kwetu ni majonzi kwa Nswima ni zaidi. BURIANI Frola. 11. Majukumu na upweke Frola umemwachia Nswima, nafsini hatakusahau ...