VIJANA WANATAKIWA KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUJIPATIA KIPATO.
NA: Franco NKYANDWALE SUMBAWANGA.
VIJANA
WANATAKIWA KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUJIPATIA KIPATO.
Vijana watakiwa kutumia mitandao
ya kijamii kujiinua kiuchumi zama hizi za teknolojia na utandawazi badala ya kukaa
vijiweni huku wakiilalamikia serikali kuwa hakuna ajira.
Hayo yameelezwa leo na Mhubiri
Enala Malila wakati wa siku ya kuadhimisha sikukuu ya vijana kwenye Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania Usharika wa Luther Dayosisi ya Ziwa Tanganyika
katika Manispaa ya Sumbawanga.
“Wapo baadhi ya vijana ambao
humiliki simu janja kubwa na zenye gharama ambazo huzitumia kuchati na kuangalia
mambo ambayo huwapotosha kimamaadili, badala ya kuzifanya simu hizo kuwa mtaji
ambapo wangewaza kutangaza biaashara zao ndogondogo wanazozifanya mitaani kwao,”
Malila alifafanua.
Mzee wa Kanisa Mariamu Ndongokazialisoma
somo la pili kutoka kwenye kitabu cha 1Timotheo 4:11-16, Mhubiri Malila
alifafanua zaidi kuwa ili kijana aweze kufanikiwa kichumi ni lazima kijana
aweze kujitambua, kukua kimwili, kiakili, kihisia, kiroho na kiuchumi kwa
kumtegemea Mungu.
Mhubiri Malila aliwashauri
vijana wenzake kuwa mitandao ya kijamii na simu janja ziwasaidie, kutafuta
ajira, kujiendeleza kitaaluma, kutangaza Neno la Mungu kwa vitendo na vijana
lazima wawe na uthubutu wenye utayari wa kufanya mambo yenye manufaa kwa jamii
badala ya kuwa na maisha hatarishi na tegemezi.
Mwongoza ibada hiyo Upendo
Msigwa alihitimishwa kwa kunukuu andiko la Biblia kutoka Mithali 4:10 alisema,
vijana ni muhimu kuchagua mambo ya kufanya kutoka kwenye mitandao ya Kijamii na
kufanya jambo kwa nia kulingana na mazingira walipo na si
kwa ulegevu ila kwa bidii na uvumilivu ili kuepukana na umasikini wa kujitakia.
Comments
Post a Comment