Kukumbatia ujuzi wa Dijitali mustakabali wa uandishi wa habari.
Kukumbatia ujuzi wa Dijitali mustakabali wa uandishi wa
habari.
Ulimwengu umeingia katika mfumo wa teknolojia
iliyokuwa ,hivyo kupelekea kuachana na mfumo wa analojia na kwenda na dijital hii
ina rahisisha namana nzuri ya mawasiliano,pamoja na upatikanaji wa taarifa mbalimabali ndani na nje ya nchi,pia ni
mabadiliko ambayo yanaendana sambamba na
ubunifu wa kidijital
Ujuzi wa kidigitali ni uwezo wa kutumia mbinu mpya
za kiteknolojia katika kutatua matatizo ya kiutendaji katika nafasi za uandishi wa habari na kupata
matokeo chanya yanayomfanya kutambulika katika ulimwengu wa digitali.
Asha Abinallah ni kiongozi wa kampuni ya media convergency inayotoa mafunzo kwa
waandishi wa habari wanawake kuhusu uandishi wa kidigitali ikiwa na lengo la
kuwaendeleza waandishi wa habari katika
uandishi wa habari kutumia teknolojia iliyokuwa.
Amesema
kupitia program hiyo maalumu ya mafunzo ya ujuzi kidigitali inawapa
waandishi kupata uelewa na ujuzi wa namna ya kuandaa na kutengeneza maudhui kwa
ajili ya kuyatumia katika majukwaa ya
kidijitali.
Abinallah ameongeza kuwa kutumia
kutumia mitandao hiyo kama majukwaa ya uandishi wa habari kwa kuandaa
vipindi,habari,makala wanavyoandaa
inasaidia kutengeneza fursa za kujiongezea kipato.
Lilian Urio ni mwandishi wa kidigitali ambaye ni mkufunzi wa mafunzo ya
uandishi wa kiditali,amesema
mwandishi wa habari anapaswa kujua stadi za kiditali ambazo ndio mwongozo
katika kuandaa maudhui pamoja na kujua namna ya kutumia majukwaa ya digitali.
,,ili
kuweza kupata habari na data kwa usahihi,
ili kuandaa maudhui bora nayanayoeleweka
kwa jamii ni lazima wandishi ukubali kubadilika na uendane na kasi ya
kukumbatia huu ujuzi wa
kidijitali,amesema Lilian Urio.
Naye peter Helatano
mwandishi wa habari anaye wakilisha global tv online Mkoani Rukwa ,amesema
ifike mahali waandishi wa habari waone umuhimu wa kukumbatia ujuzu huu wa
dijitali kwa kuwa kunafursa nyingi kwa
mwanahabari ambazo zitawaongezea ujuzi,,amesema kupitia simu janja anayotumia
inaweza kufanya vitu vingi sana amesema ndio ofisi yake anayotumia kupata habari,na kutuma habari
anazoandaa.
ANNA MALISA
Comments
Post a Comment