JARIBIO LA ZOEZI LA SENSA KUFANYIKA RUKWA

 


Na: FRANCO NKYANDWALE:. SUMBAWANGA.

 

Wananchi Mkoani Rukwa wametakiwa kujiandaa na zoezi la sensa litakalofanyika Mwezi Agost 23 mwaka huu kwa kuwepo kwenye kaya zao ili watoe ushirikiano kwa makarani wa sensa ili wahesabiwe kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.


Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa kijiji cha Luwa Kata ya Ntendo katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Saveri James alipokuwa akiongea na Rukwa press wakati makarani wa sensa walipotembelea kijijini hapo kwa lengo la kukagua miundo mbinu mbalimbali na mipaka ya kijiji.

James amesema kuwa sensa ya watu na makazi ni muhimu kwa taifa lolote ambalo linaweka mipango na mahitaji muhimu kwa jamii yake na lengo la sensa hiyo ni kujua idadi ya watu na makazi na kuweka mipango ya namna serikali itakavyoendesha shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kuboresha miundo mbinu kwa manufaa ya wananchi. 


Kwa upande wa baadhi ya wananchi wamesema wao wamejiandaa kuhesabiwa ambapo Mwanakijiji  Leonard Mikael ameshuhudia kuwa wapo tayari kuhesabiwa na kuwamasisisha hata wale watakaosuasua kuhesabiwa kutokana na uelewa mdogo juu ya manufaa ya sensa ya watu na makazi.

Comments

Popular posts from this blog

Wakulima Rukwa kutumia zana bora kuongeza uzalishaji wa mazao msimu mpya wa kilimo

UTPC KUENDELEA KUELIMISHA UMMA,UMUHIMU WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

MAENDELEO YA CHUO CHA UALIMU SUMBAWANGA