JIPANGENI ZAIDI KUHAKIKISHA WATU WANAJITOKEZA SIKU YA SENSA-ANNE MAKINDA-KAMISAA WA SENSA TANZANIA
Kamisaa wa sensa na
Spika Mstaafu Anne Makinda amewataka viongozi wa mkoa wa Rukwa kujipanga
kuhakikisha watu wengi zaidi wanajitokeza siku ya kuhesabiwa ifikapo Agosti 23
mwaka huu nchi itakapofanya zoezi la sensa ya watu na makazi.
Kiongozi huyo ametoa
wito huo mjini Sumbawanga wakati akizungumza na wadau kuhusu hali ya
maandalizi ya sensa nchini pamoja na kutoa elimu ya umuhimu wa zoezi la sensa
mwaka huu 2022.
Makinda alibainisha
kuwa katika zoezi zoezi hili limejengwa katika msingi wa kiutawala ambapo
utaratibu umewekwa watu watahesabiwa pale alipolala.
" Tutahesabu watu
wote mahala walipolala kama ni vituo vya mabasi, nyumba za wageni, katika kaya,
waliopo hospitalini pia wale watakaokuwa kwenye magereza na mahabusu wote
maharani wa sensa watawafikia kwa utaratibu uliowekwa na serikali"
alisisitiza Mama Makinda.
Katika hatua nyingine
Kamisaa huyo wa sensa alisema viongozi na jamii ya mkoa wa Rukwa ikumbuke
umuhimu wa kutoa taarifa za walemavu Ili nao wahesabiwe kwenye sensa hatua
itakayosaidia serikali kujua idadi yao na hali zao kuwezesha upatikanaji wa
huduma stahiki.
Kamisaa huyo alishauri
viongozi wa mkoa wa Rukwa kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya zoezi hili
ambapo ametaka wawaandae wananchi kushiriki ipasavyo katika kutoa majibu kwa
maswali watakayoulizwa na makarani wa sensa Ikiwemo kuandaa vitambulisho au
namba NIDA .
Naye Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa Joseph Mkirikiti alisema kwa juwamkoa huo upo mpakani tayari vyombo ya
dola vimejiandaa kushirikiana na wataalam kufanikisha zoezi la sensa ili
raia wanaostahili kuhesabiwa wajItokeze huku ulinzi ukiimarishwa.
"Sensa ni takwa
la kisheria tutasimamia vema,licha ya mkoa wetu kuwa mpakani tumejipanga kusimamia
zoezi hili kwa kutumia vyombo vyetu ya ulinzi na usalama " alisisitiza
Mkirikiti.
Mkirikiti alitoa rai
kwa vyombo vya habari hususan radio za kijamii zikizopo mkoa wa Rukwa kutoa
nafsi kwa wataalam wa sensa na viongozi kutoa elimu na hamasa juu ya
sensa ya watu na makazi ili wananfhi wengi wapate uelewana hatumaye wajitokeze
siku ya kuhesabiwa.
Akitoa taarifa kuhusu
maandalizi ya sensa ngazi mkoa,Mratibu wa mkoa Adam Ramadhan alisema tayari
vituo vya kuhesabia watu 2,190 vimeandaliwa kwenye halmashauri nne za
Sumbawanga Manispaa, Sumbawanga vijijini,Nkasi na Kalambo.
Kamisaa wa Sensa ya
Watu na Makazi Mama Anne Makinda anendelea na ziara yaje ya kutoa elimu na
hamasa ya sensa ambapo leo pia atazungumza kwenye mkutano wa hadhara kiiji cha
Kasanga wilaya ya Kalambo.
Comments
Post a Comment