VIJANA WA KIKRISTO WATAKIWA KUWA KIELELEZO KWA JAMII



 NA: FRANCO NKYANDWALE SUMBAWANGA.


Mwalimu Kitaaluma Joseph Shilingi wa Kanisa la Evangelist of God (T) Mashujaa wa Yesu Pito lililopo katika Halimashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ameyasema hayo wakati wa semina ya Vijana inayoendelea Kanisani hapo kuanzia Jumapili ambayo itakachukua muda siku tatu zaidi. 

Amewataja Vijana kuwa ni nguzo muhimu ya Kanisa na kwa jamii kwa ujumla, amesema kuwa wapo baadhi ya Vijana wamejificha Kanisani na kufanya vitendo ambavyo havimpendezi Mungu.

Mwalimu Shilingi amewashauri wazee wa Kanisa kufuatilia mwenendo wa Vijana ambao hawana msimamo wa imani ya kikristo wakalishwe chini na kuonywa mapema bila kufanya hivyo hapatakuwa na ndoa imara hapo baadaye na Kanisa litapoteza mwelekeo.

Msingi wa Kanisa lolote ni kuwa na wakristo waliosimama kiroho, kimwili, kiuchumi, na kumtumikia Mungu wakiwa wasafi wa miili na mazingira yao kimaisha.

Mwalimu Shilingi alisisitiza na kufafanua kwamba Vijana wajishulishe na biashara ndogo ndogo ili wasiwe tegemezi katika familia zao baada ya masomo na wanaposubiri ajira, aidha alionya kuwa baadhi ya wasichana hujihusisha na vitendo vya kujiuuza ili wajipatie kipato ambacho ni haramu na wajitambue kuwa yapo maradhi yasiyo na tiba.

Pamoja na hayo aliwashauri wazazi wanaoshiriki semina hiyo kushirikiana na Walimu katika kuwalea wanafunzi ili wasiwe watoro shuleni hasa wale wa Shule ya Msingi ambako ni mwanzo kujua Kusoma, kuhesabu na kuandika ambao baadaye watoto hao huwa ni watumishi wa Kanisa na wananchi wazalendo.

Nb. Picha 1. Mwalimu Kitaaluma Joseph Shilingi akiendesha semina Kanisani huko Pito.
Picha 2. Katibu Hamis KIBONA wa Kanisa hilo akitoa matangazo.

Comments

Popular posts from this blog

Wakulima Rukwa kutumia zana bora kuongeza uzalishaji wa mazao msimu mpya wa kilimo

UTPC KUENDELEA KUELIMISHA UMMA,UMUHIMU WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

MAENDELEO YA CHUO CHA UALIMU SUMBAWANGA