Karibu Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote
Karibu Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Wapendwa watanzania wenzangu, Ili kufanikisha dira yetu ya: “Kufanikisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano Tanzania kikamilifu na kwa usawa”, Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) unalenga kuimarisha uwezo wa kushirikiana na watoa huduma za mawasiliano nchini ili kuhakikisha ufikiaji wa huduma za mawasiliano katika maeneo yote yenye mawasiliano hafifu pamoja na yale yasiyo na huduma hiyo kabisa. Katika kutekeleza majukumu yake, Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) umejielekeza katika kubaini maeneo ya miradi ya mawasiliano ambayo yanaweza kupata ruzuku Serikalini kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, lengo ni kuhakikisha wananchi wote wanafikiwa na huduma za mawasiliano ambayo kwa kiasi kikubwa yanachangia katika uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na Serikali kwa ujumla. Tangu kuanza kazi kwa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) mwaka 2009, kumekuwa na mafanikio mengi katika sekta ya mawasiliano, ...
Comments
Post a Comment