MRATIBU MSAIDIZI WA SENSA MKOANI RUKWA JAMES KAPENULO AKIELEZEA MATUMIZI YA VISHIKWAMBI KWA WAANDISHI WA HABARI
NA: FRANCO NKYANDWALE. SUMBAWANGA. Mratibu Msaidizi wa Sensa ya Watu na Makazi Mkoani Rukwa James Kapenulo akielezea matumizi ya vishikwambi kwa Wandishi wa Habari Mkoani Rukwa, amesema kuwa vishikwambi hivvyo vitatumika na makarani wa Sensa hiyo hapo tarehe 23.08.2022 na Makarani hao watapatiwa mafunzo jinsi ya kuvitumia na amefafanua kwamba, zoezi hilo ambalo litafanyika kidigitali na ni Sensa ya tofauti ikilinganishwa na Sensa zote zilizofanyika hapo awali. Ambapo taarifa za Kidemografia zitajazwa kwenye mfumo kupitia kishikwambi hali itakayoondoa upotevu wa taarifa muhimu za watu.