KIKUNDI CHA WAVUVI KATA YA SAMAZI CHAPATA MKOPO WA BOTI NA ZANA ZA UVUVI
Wizara ya Mifugo na uvuvi kupitia Benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania TDB imesaini Mkataba wa mkopo wa boti ya uvuvi na zana za uvuvi Kwa kikundi Cha uvuvi Cha Umoja kilichopo kata ya Samazi Wilaya ya Kalambo Mkoa wa Rukwa kama hatua yakuwawezesha wavuvi kujikwamua kiuchumi. Akiongea ofisini kwake wakati wa hafla fupi ya kusaini Mkataba huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kalambo Shafi Mpemba,amesema mkopo huo una thamani ya Shilingi Milioni thelathini na Saba na kwamba umetolewa kwa ajili ya ununuzi wa boti aina ya Fiber,nyavu,mashine na kifaa Cha kutafutia samaki ziwani. Licha ya Hilo Mpenda aliipongeza Serikali ya awamu ya sita kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa mkopo huo pamoja na boti mbili zenye thamani ya milioni 108 ambazo kwa pamoja zinaenda kusaidia kudhibiti uvuvi haramu,Udhibiti na usimamizi wa rasilimali uvuvi katika kata ya Kasanga na Samazi katika mwambao wa Ziwa Tanganyika. Kwa upande wake diwani wa kat...