RUKWA YAPONGEZWA MAANDALIZI YA UDTHIBITI POLIO
Mganga Mkuu wa Serikali Pro.Tumain Nagu ameipongeza timu ya uendeshaji wa Huduma za Afya ngazi ya Mkoa (RHMT) ya Mkoa wa Rukwa kwa maandalizi na hatua za haraka zilizochukuliwa baada ya kisa kimoja Cha Polio kuripotiwa hapo tarehe 26 Mei ,2023.
Ameyazungumza hayo Leo Septemba 14,2023 alipofanya kikao na timu ya uendeshaji wa Huduma za Afya ngazi ya Mkoa (RHMT) wakati wa kujadili na kukagua maandalizi ya Mkoa wa Rukwa kutoa chanjo dhidi ya polio
Mganga Mkuu wa Serikali atafanya ziara katika Halmashauri ya Manispaa Sumbawanga ambapo atatembelea kituo Cha Afya Mazwi na Zahanati ya kilimahewa,pia atatembelea Halmashauri ya Wilaya Nkasi ambapo atatembelea hospitali ya Wilaya ya Nkasi na kituo Cha Afya Nkomolo.
Profesa Nagu,amesisitiza kuwa watoto 391,883 walilengwa wapatiwe chanjo ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa Polio ugonjwa huo ambao unaathiri watoto chini ya umri wa miaka 05 hadi 15.
Comments
Post a Comment