WATOTO 391,883 KUPATIWA CHANJO YA POLIO RUKWA
Watoto 391,883 wenye umri chini ya miaka name wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa Polio.
Kampeni hii ni maalumu kwa watoto waliozaliwa kuanzia mwaka 2016,Kampeni hii inakuja baada ya kuthibitika kwa kisa Cha Polio kwa mtoto Mmoja Manispaa ya Sumbawanga
Akifungua kikao Cha kamati ya Afya ya Mkoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Rukwa Mh.Lazaro Komba Mkuu wa wilaya Kalambo,amesema kuwa ugonjwa wa Polio unazuilika kwa kuwapatia chanjo watoto wote wenye umri chini ya miaka nane.
Amewasisitiza kuwa wazazi na walezi kutoa taarifa katika vituo vya afya iwapo wataona dalili za watoto kupooza ghafla.Amehimiza jamii kuzingatia kanuni za Afya hasa kwa kunawa mikono kwa Maji safi yanayotiririka na kuagiza Kila kaya kuwa na choo Bora na kukitumia choo hicho ipasavyo ili kupunguza maambukizi ya magonjwa.
Amewataka wazazi,walezi,viongozi wa dini na viongozi wa kimila kutoa ushirikiano kwa wataalamu wa Afya watakaokuwa wakitoa chanjo nyumba kwa nyumba,vituo vya Afya,katika mikusanyiko ya watu,katika nyumba za ibada na Shuleni.
Comments
Post a Comment