WANAFUNZI 7,522 WATARAJIA KUFANTA MTIHANI WA KUMALIZA DARASA LA SABA WILAYA YA KALAMBO
Mkuu wa wilaya Kalambo Mkoa wa Rukwa Lazaro Komba amesema wanafunzi 7,522 kati Yao wavulana wakiwa 3,404 na wasichana 4,118 wanatarajia kuanza kufanya mtihani wakumaliza Elimu ya msingi Wilayani Kalambo na kuwaonya vikali wasimamizi watakao bainika kuvujisha mitihani na kwamba Sheria Kali zitachukuliwa dhidi Yao.
Aidha Komba amesema mitihani hiyo itafanyika kwenye vituo 330 kupitia shule 98 za Wilaya hiyo na Kila mkondo utakuwa na idadi ya watahiniwa 25 na kuwaonya vikali wazazi na walezi watakaobainika kujihusisha na tabia za kuwalaghai watoto wao kwa kuwazuia kufanya vizuri mitihani Yao kwa Nia ya kuwaozesha na kwamba Sheria Kali dhidi Yao zitachukuliwa.
Hata hivyo kwa mujibu wa Afisa Elimu Mkoa wa Rukwa Samson Hango,amesema idadi ya watahiniwa kwa mwaka 2023 ni 32,217 ambapo imepungua kwa jumla ya watahiniwa 1,227 sawa na asilimia 3.8% ikilinganishwa na watahiniwa 33,444 waliosajiliwa mwaka 2022.
Comments
Post a Comment