MPANGO WA UHAMASISHAJI WA USAJILI WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO KUZINDULIWA

 Wakala wa Usajili,ufilisi,na udhamini Nchini(RITA)unatarajia kuzindua mpango wa uhamasishaji wa usajili wa watoto chini ya miaka mitano ili waweze kupatiwa vyeti vya kuzaliwa.


Hayo yamebainishwa kupitia Semina ya siku Moja iliyofanyika mkoani Kigoma ikihusisha viongozi waandamizi wa Serikali ikiwa ni pamoja na Katibu Tawala Mkoa,Makatibu Tawala Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri,Kamati ya Usalama Mkoa,Viongozi wa dini na wazee maarufu ili kuweza kutumia nafasi zao kuhamasisha jamii kushiriki kwenye zoezi Hilo.



Naibu kadhi Wasii Mkuu Irene Lesulie amesema kuwa mpango huo unaolenga kusajili na kutoa vyeti kwa watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano waliozaliwa Nchini kutokana na idadi ndogo ya watoto waliosajiliwa na kupata vyeti ikilinganishwa na idadi halisi ya waliozaliwa. 



Comments

Popular posts from this blog

Wakulima Rukwa kutumia zana bora kuongeza uzalishaji wa mazao msimu mpya wa kilimo

UTPC KUENDELEA KUELIMISHA UMMA,UMUHIMU WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

MAENDELEO YA CHUO CHA UALIMU SUMBAWANGA