WAKULIMA NA WAFANYA BIASHARA KUJITANGAZA KITAIFA NA KIMATAIFA
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Be.Gerlad Mweli ametoa wito wa wakulima na wadau wa kilimo kutumia Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika 2023 (AGRF)katika kujitangaza ili kuweza kunufaika na fursa za masoko ya ndani na nje ya nchi.
Katibu Mkuu Mweli alikuwa anajibu swali lililoulizwa na miongoni mwa washiriki katika mkutano wa pembezoni mwa Jukwaa la Mifumo ya Chakula 2023 katika kikao Cha pamoja na Mawaziri na Makatibu wakuu kutoka Wizara za kilimo,Mifugo na uvuvi,Uchumi wa Buluu Zanzibar,kilimo ,ufugaji,umwagiliaji na italii Zanzibar pamoja na wadau wa kilimo.
Bw.Mweli aliongeza na kusema kuwa wakulima watumie fursa mbalimbali za majadiliano yaliyoanza tarehe 5-8 Septemba 2023 ili kujifunza,kubadilishana mawazo,kutangaza bidhaa na kuvutia italii na wawekezaji kwenye kilimo,na kutafuta masoko nje ya nchi.
Wakulima na wafanya biashara wa mazao wamehamasishwa kutumia Jukwaa la kimtandao lijulikanalo Kama "M-kilimo"ambalo linawakutanisha wauzaji na wanunuzi kupata masoko kwa njia ya mtandao.
Ameongeza kuwa Tanzania itaendelea kuratibu majukwaa mbalimbali ya kilimo,huku Jukwaa hili la AGRF 2023 likilengwa kuwa endelevu ili kutoa fursa ya kuwakutanisha wakulima,wafanyabiashara,wawekezaji na Taasisi mbalimbali za fedha kunufaika na sekta ya kilimo Nchini.
Comments
Post a Comment