SERIKALI KUANZA KUTUMIA MFUMO MPYA WA NEST KUFANYA MANUNUZI YA UMMA

 Mafunzo rasmi ya siku Tano Leo,wataalamu kutoka Halmashauri za Mkoa wa Rukwa ya Mfumo mpya wa manunuzi wa umma kielektroniki NeST ili waweze kufanya manunuzi kupitia mfumo huo mpya ulioboreshwa zaidi.

Akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa TEHAMA Mkoa wa Rukwa Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Masuala ya Utumishi na rasilimali watu Mkoa wa Rukwa Ndg.Donald Nssoko ambapo ameeleza kuwa Mafunzo hayo yatasaidia Usimamizi wa Sheria ya manunuzi, Kuongeza uwazi na kuzuia masuala ya Rushwa katika Mchakato wa manunuzi.

Aidha amewataka Makatibu Tawala wasaidizi pamoja na wakuu wa vitengo ofisini hapo kuteua watumishi sahihi kutoka kwenye idara zote kama miongozo inavyoelekeza katika Matumizi sahihi ya Mfumo mpya wa NeST.

Kwa upande wake Mkaguzi wa ndani Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa Ndg.Godfrey Haule amesisitiza kujenga umakini katika kutumia Mfumo huo mpya utakaosaidia kuepusha hoja zisizo nzuri za ukaguzi zinazojitokeza kutokana na Makosa ya kutumia Mfumo.

Mafunzo ya Mfumo wa NeST yatatolewa pia kwa watumishi ngazi ya Halmashauri Mkoa wa Rukwa ili waweze kuanza mara Moja kutumia Mfumo huo mpya wa ununuzi wa umma.

Awali Serikali ilikuwa ikitumia Mfumo wa TANEPS katika ununuzi wa umma ambao ulibainika kuwa na changamoto mbalimbali hatua iliyopelekea Serikali kuachana na Mfumo wa zamani na kuja na Mfumo wa NeST ili kurekebisha changamoto zilizojitokeza na kuboresha Mfumo mzima wa ununuzi wa umma.


Comments

Popular posts from this blog

Wakulima Rukwa kutumia zana bora kuongeza uzalishaji wa mazao msimu mpya wa kilimo

UTPC KUENDELEA KUELIMISHA UMMA,UMUHIMU WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

MAENDELEO YA CHUO CHA UALIMU SUMBAWANGA