MWENYEKITI WA CCM MKOA WA RUKWA AMPONGEZA MBUNGE KATIKA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM JIMBO LA KWELA.

 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Rukwa Bi.Sirafu Maufi apongeza taarifa ya tathimini ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ndani ya miaka mitatu ya Wilaya ya Sumbawanga vijijini iliyowasilishwa na Mbunge wa Jimbo la Kwela Mheshimiwa Deus Clement Sangu katika Mkutano wa Halmashauri kuu Wilayani humo.


"Ninashukuru na kumpongeza Mbunge kwa kazi nzuri aliyoifanya ya utekelezaji wa Ilani ya Chama kwa kipindi Cha miaka mitatu iliyosimamiwa,kufuatiliwa na kutekeleza chini ya Uongozi wa Jimbo la Kwela ameonesha umahiri na uzalendo katika Jimbo lake la Kwela".Amesema Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Rukwa.



Aidha Bi. Sirafu Maufi amewataka wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Wilayani humo kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Nae Mbunge wa Jimbo la Kwela Mheshimiwa Deus Sangu amesema kupitia fedha walizopata kutoka Serikali kuu wamefanikiwa kujenga kituo Cha Afya Kipeta na kupitia Mapato ya ndani ya Halmashauri tumejenga kituo Cha Afya kaoze tupo katika hatua za mwisho,na kituo Cha tatu tumejenga katika Kijiji Cha   kaengesa .Pia tumejengewa shule mbili za  sekondari katika kata ya Nankanga na kata y ya Laela, Katula sekondari.Tunatarajia  katika mwaka ujao wa fedha kujenga vituo viwili vya Afya.



"Katika Tarafa ya Laela Mji mdogo wa Laela kumekuwa na changamoto ya Maji hivyo katika Bilioni 14 zilizotolewa na Serikali  tunaenda kufanya upembuzi yakinifu  wakuchukua Maji katika mto Momba ambao utapeleka Maji kata ya Miangalua,Laela,Mlokola na Lusaka na hizi juhudi za maendeleo zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan."Amesema Mh.Sangu.

Aidha Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Sumbawanga vijijini wamekiri kuridhishwa na utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi unaoendelea katika Wilaya hiyo.






Comments

Popular posts from this blog

Wakulima Rukwa kutumia zana bora kuongeza uzalishaji wa mazao msimu mpya wa kilimo

UTPC KUENDELEA KUELIMISHA UMMA,UMUHIMU WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

MAENDELEO YA CHUO CHA UALIMU SUMBAWANGA