Ni miezi kadhaa tangu Mh mnanka kuchaguliwa kwake na wananchi wa kata ya msuwa ili aiongoze kata hiyo na kufikia malengo huku changamoto mbalimbali kama vile shule,barabara na maji vikiwa vikwazo katika kata hiyo.Leo ni mkutano wake muhimu wa kueleza mpango kazi na mikakati ya kuhakikisha kata hiyo inakuwa na maendeleo swali kubwa kwa wananchi ni kuhusu ukarabati wa barabara za mitaa kwaani imekuwa kero kubwa kwa wananchi kata hiyo Mh. Mnanka anawaasa wenyekiti wa mitaa kushugulikia barabara za mitaa yao ili ziingie kwenye mfumo zitambuliwe na hatimaye kukarabatiwa Kero nyingine kubwa ni shule kwani watoto wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kufata masomo yao hali iliyopelekea mh diwani kukaa na wananchi wake kuamua kuchangia ili waanze ujenzi wa shule,wananchi nao wameitikia wito na kutoa maoni yao juu ya ujenzi wa shule kuwa uendelee kwa kuchangia kila Kaya ili kuanza ujenzi wa vyumba vya madarasa.