Being,China -Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU)inashiriki kongamano la 5 la kimataifa la mashirikiano katika mapambano dhidi ya rushwa,linaloendelea jijini Beijing China. Kongamano hili limewakutanisha mamlaka 219 kutoka nchi 121 duniani,likilenga kubafilishana uzoefu na utaalamu katika jukumu la kuzuia na kupambana na rushwa Kongamano hili la siku Tano limejumuisha warsha ya viongozi wa mamlaka za kuzuia na kupambana na rushwa(high level Forum),ambapo Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU ,Bw.Crispin Francis Chalamila,amewasilisha mada kuhusu "mfumo wa Sheria wa Tanzania katika mapambano dhidi ya rushwa"katika mada yake Bw.Chalamila ameeleza jinsi ambavyo serikali ya Tanzania imekuwa ikijipambanua katika mapambano dhidi ya rushwa kwa kuimarisha mifumo ya Sheria na ya kitaasisi.Alibainisha uanzishwaji wa divisheni ya mahakama kuu inayoshughulikia masuala ya rushwa na uhujumu uchumi kuwa ni hatua muhimu katika kuhakikisha uwajibikaji na utawala Bora. TAKUKURU...
RC SENDIGA: TUTAFANYA MAPINDUZI YA KILIMO RUKWA Na. OMM Rukwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga amesema anatamani kuona mkoa wa Rukwa ukifanya mapinduzi makubwa katika sekta ya kilimo kiwe cha kibiashara na kukuza uchumi wa wananchi. Ili kufanikisha hilo amewataka wataalam wa kilimo katika halmashauri zote nne za Rukwa kuja na mikakati ya kufanya kilimo kichangie zaidi katika kukuza pato la wananchi na kuongeza uhakika wa chakula. Mkuu huyo wa Mkoa amesema hayo jana mjini Sumbawanga (10 Agosti, 2022) wakati wa hafla rasmi ya makabidhiano ya ofisi toka kwa mtangulizi wake Joseph Mkirikiti kufuatia Rais Samia Suluhu Hassan kumteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. “Natamani kuiona Rukwa ikifanya mapinduzi makubwa katika kilimo. Maafisa kilimo na ugani jitahidini kuwa na mipango mizuri ili kilimo chetu kiwe cha kibiashara na kuhusisha vijana wengi “alisema Sendiga. Sendiga aliongeza kusema mkoa lazima uwe na mkakati wa kufanya vijana wengi kurudi vijijini ili kufanya ...
Hayati Mpendwa mzee wetu Dk. Chrisant Mzindakaya mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania aliyefariki katika hospitali ya Mhimbili jijini Dar es salaam alikokuwa akitibiwa anatajarajiwa kuzikwa Alhamisi Juni 12,2021 mida ya saa 9 Alasiri. Msemaji wa familia Frank Mzindakaya amesema Mzindakaya kabla hajafariki alitoa maelekezo ywa mahali pa kuzikiwa akifa.Hivyo familia itatekeleza jambo hilo.Hayati mzee wetu Dk. Mzindakaya anashikilia rekodi ya kuwa kiongozi aliyedumu katika uongozi kwa mda mrefu rekodi ambayo bado haijavunjwa na mtu yoyote hapa nchini kwa takribani miaka 40.Pumzika kwa amani mzee wetu tutaenzi mema na ushauri wako katika kulijenga Taifa letu la Tanzania.Imeandaliwa na Peter Helatano
Comments
Post a Comment