WALIOFUKUA KABURI WAKAMATWA NA JESHI LA POLISI RUKWA

 

Jeshi la Polisi mkoani Rukwa linawashikilia watu watatu wote wakazi wa Kirando wilayani Nkasi kwa tuhuma ya kufukua kaburi la marehemu asiyefahamika jina lake na kukata kichwa chake kisha kwenda kukitelekeza kwenye kichanja cha kuanikia vyombo nje ya nyumba ya mkazi mmoja wa kijiji cha Kirando Mkoani Rukwa.

 Regina Samwel  katika maelezo yake anadai aliamka kwenda uani lakini  anakutana na harufu kali isiyoyakawaida hivyo alirudi ndani kumwarifu mamake  aliyetoka nje  na kukuta kichwa cha binadamu kimehifadhiwa kwenye sufuria juu ya kichanja cha vyombo kilichopo nje ya nymba yao.


 




Katika uchunguzi wa awali wa Polisi katika eneo la Kirando walifanikiwa kumkamata mtu mmoja kutokana na mfanano wa nyayo zake zilizoonekana kwenye eneo la tukio na hata kwenye kaburi hilo, hali iliyowashangaza hata wakazi wa eneo hilo wakidai kuwa hawajawahi ona tukio la aina hiyo maisha mwao.

Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa William Mwampaghale amesema licha ya kuwakamata watu hao, bado uchunguzi unaendelea kufahamu kwanini walifanya hivyo.

Bado haijawekwa wazi kuwa ni kwanini watuhumiwa hao walifukua kaburi na kukata kichwa hicho japokuwa baadhi ya wakazi wa eneo hilo wanahusisha kitendo hicho na imani za kishirikina


Comments

Popular posts from this blog

Wakulima Rukwa kutumia zana bora kuongeza uzalishaji wa mazao msimu mpya wa kilimo

UTPC KUENDELEA KUELIMISHA UMMA,UMUHIMU WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

MAENDELEO YA CHUO CHA UALIMU SUMBAWANGA