TUJITOE TUJENGE SHULE YETU,KERO YA BARABARA ZA MITAA WENYEVITI ZIWEKENI WEZI ZITANBULIKE KWENYE MFUMO


 

Ni miezi kadhaa tangu Mh mnanka kuchaguliwa kwake na wananchi wa kata ya msuwa ili aiongoze kata hiyo na kufikia malengo huku changamoto mbalimbali kama vile shule,barabara na maji vikiwa vikwazo katika kata hiyo.Leo ni mkutano wake muhimu wa kueleza mpango kazi na mikakati ya kuhakikisha kata hiyo inakuwa na maendeleo swali kubwa kwa wananchi ni kuhusu ukarabati wa barabara za mitaa kwaani imekuwa kero kubwa kwa wananchi kata hiyo

Mh. Mnanka anawaasa wenyekiti wa  mitaa kushugulikia barabara za mitaa yao ili ziingie kwenye mfumo  zitambuliwe na hatimaye kukarabatiwa

Kero nyingine kubwa ni shule kwani watoto wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kufata masomo yao hali iliyopelekea  mh diwani kukaa na wananchi wake kuamua kuchangia ili waanze ujenzi wa shule,wananchi nao wameitikia wito na  kutoa maoni yao juu ya ujenzi wa shule kuwa uendelee kwa kuchangia kila Kaya ili kuanza ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Comments

Popular posts from this blog

Wakulima Rukwa kutumia zana bora kuongeza uzalishaji wa mazao msimu mpya wa kilimo

UTPC KUENDELEA KUELIMISHA UMMA,UMUHIMU WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

MAENDELEO YA CHUO CHA UALIMU SUMBAWANGA